ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 13, 2015

Ukatili ulioje!

Polisi wakiwa katika eneo la tukio.

KWELI ni ukatili! Mwanamke mmoja anayesemekana kuwa ni mke wa mtu anadaiwa kuhusika katika kumtumbukiza kichanga wake kwenye choo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwanzo Mgumu, Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.
Nyuma ya askari polisi ni choo alimotupwa mtoto huyo.

Ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita ndani ya choo hicho ambacho pia kipo jirani na kambi ya wanawake wanaojiuza miili ‘machangudoa’.

Paparazi wetu alifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya watu kukusanyika na kukuta wakishangaa tukio hilo huku wengine wakiliita ni la kikatili kufanywa na mwanamke aliyelea mimba kwa tabu kwa muda wa miezi tisa.

Ofisi ya serikali ya Mtaa Mwanzo Mgumu katika Manispaa ya Morogoro.

“Yaani kusema ukweli mi naona kama mwanamke unaona mambo ya kulea huyapendi, basi afadhali usishike mimba. Lakini kusubiri mpaka mtoto amezaliwa halafu unamtumbukiza chooni, ni ukatili mkubwa sana,” alisikika akisema mwanamke mmoja shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stamili Juma Liwawa.

Akaongeza: “Mimi mwenyewe nina watoto watatu, kila mmoja na baba yake lakini sijamtupa hata mmoja. Nilikomaa na Vicoba, wakasoma mpaka sasa ni wakubwa.

“Mimi kama ningemwona huyu mwanamke kwa kweli ningempiga bila kujali sheria. Ukatili huu si wa kufanywa na mama kwa mtoto wake mwenyewe.”

Baada ya kuona polisi hawajafika, Amani liliwapigia simu ambapo baada ya muda walifika na kukichukua kichanga hicho hadi Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya taratibu nyingine.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilitaka jeshi la polisi mkoani hapa kumsaka mwanamke aliyetupa mtoto huyo kwa vile kuna watu wanasema wanamfahamu kwa kigezo kwamba, alipokuwa mjamzito walimwona lakini kwa sasa hana tumbo na wala hawana taarifa za kufiwa na kichanga baada ya kujifungua.

Wengine walikwenda mbele zaidi kwa kushauri kuwa, kambi ya machangudoa iliyopo eneo linalojulikana kwa jina la Itigi ingeondolewa mara moja kwani huenda mhusika alitoka hapo.

No comments: