ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 27, 2015

YALIYOJIRI KATIKA KONGAMANO LA BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA LEO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono baadhi ya Wanawake wanachama wa CHADEMA, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee akizungumza na Umati wa Kinamama wa Chama hicho, uliokuwa umefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza hilo, uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).

Wakinamama hao wakimshangilia Mh. Lowassa na Babu Duni wakati walipowasili Ukumbini hapo.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akiwasalimia kina mama hao ambao walikosa nafasi ndani ya Ukumbi na kuamua kukaa nje.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia kina mama hao.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la BAWICHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza hilo.
Mh. Lowassa na Ujumbe wake wakiwasili Ukumbini.
Salam kwa Wajumbe.
Baadhi ya Wadau wa Sanaa ya Filamu nchini waliokuwepo kwenye Mkutano huo wa BAWICHA.
Shangwe Ukumbini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiteta jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mwenza, Dkt. Juma Haji Duni, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015.
Mmoja wa Kinamama wanaowakilisha Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee  akifatilia Hotuba ya Mama anaewakilisha Watu wenye Ulemavu.
Mh. Kaihula na Kinamamam wenzake wakifatilia Mkutano huo.
Viongozi wa Kuu.
Keki ya Siku ya Kuzaliwa kwa Mh. Lowassa iliyotolewa na Baadhi ya Washanii wanaomuunga Mkono.
Mmoja wa Wasanii wa Filamu nchini, Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea Keki ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa Msanii wa Filamu nchini, Aunt Ezekiel.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Msanii wa Filamu nchini,  Jacqueline Wolper.
 Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wenzake.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).
Mh. Lowassa katika tabasamu.
Babu Duni akifatilia jambo kwa umakini.
Mh. Mbowe na Mh. Lowassa wakiteta jambo.
Mh. Mbatia na Mh. Silima wakiteta.
Taswira mbali mbali katika Mkutano huo.
Mh. Lowassa akimpongeza Mkewe kwa hotuba nzuri aliyoitoa.
Msanii na Muziki wa Injili, Florah Mbasha akitoa burudani.



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.


Mh. Mbatia akizungumza.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa ,akitoa salamu ya Chama kabla ya hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee wakati akilihutubia Baraza hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa ,akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.

13 comments:

Anonymous said...

kweli ukawa ni zimo la taka!!!! daah mpaka na huyu muimba kwaya aliyezaa na mchungaji yumo. sasa ndio tunaona nini maana ya ukawa na viongozi wake.

Anonymous said...

Wee mdau hapo juu wacha kejeli zako za kipuuzi kama TRUMP,ccm ndio shimo la taka mpaka kina wema wanagombania ubunge,yeaaaa how about that??booo you

Anonymous said...

Wewe uliyetoa haya maoni, uchafu wa roho yako unaweza kuwa mbaya zaidi ya huyo unayemhukumu. Ondoa kwanza boriti lililoko ndani ya jicho lako ndipo utaweza kuona kibanzi kwa mwenzako. Hao wahuni wanaokata majukwaa wakifurahisha ccm ndio unawaona watu siyo.

Anonymous said...

Asiyekuwa na kosa na awe wa kwanza kurusha jiwe!!!!!

Anonymous said...

Kwani hukujua hili nalo. Na bado shimo halijaa taka bado......UKAWA hoyeeeeeee

Anonymous said...

Please, tunahitaji audio ya speech ya Lowasa kwenye hafla hii.

Anonymous said...

Naomba uwe na adabu wewe LOFA hapo juu... Naona mwenye blogu kaachia comment yako wakati anapiga kelele kuhusu matusi ila wenyewe mnaachiana kwa kuandika UPUPU hapo ����������������

Daniel said...

Acha rumous wewe nani kakwambia hayo? Nani kakwambia kazaa na mchungaji. Huna ushahidi hata kidogo

Anonymous said...

Shimo la taka ni wema tena la taka haswa kila anayekuja na uchafu wake anatumbukiza kwake,anajipendekeza na ccm na itamchafua haswa,anatafuta kuipewa uongozi wa kuuza sura kazi kwake.

Anonymous said...

Mengi yatawatoka, Watatapatapa sana na bado, peopele.............Lowasa mabadiliko, mabadiliko lowasa

Anonymous said...

neno moja Fisadi

Anonymous said...

We kilaza kweli, mmeanza kutapatapa eti mmezuiwa kutumia uwanja wa jangwani?!!! Wakati mmefoji barua ili wananchi wawaonee huruma kama vile mnaonewa!!! Wezi utawajua tu na watanzania wameshaanza kuwashtukia. Tusubiri hiyo kesho huyo papaa na speech aliyoandikiwa kama ataweza kuisoma, ilimshinda ile ya kujitangaza amejiunga na chama alichokinunua!!!!! Sasa demu wa bongo movie anaye mapeshee kulia na kushoto hamumuoni zaidi ya wema, kwenye ondoa boriti kabla hujatia kibanzi. Acheni ushabiki na kuwa bendera fuata upepo juzi kati hapa mlimuita fisadi sasa ni msafi!!!!! Mtamaafisha sana na madodoki na sabuni ya foma lakini hatakati. Magufuli hana haja kulipa fadhila maana hajachaguliwa kwa rushwa kama papaa. Eti bawacha wakati kiongozi unamuona jinsi alivyo??!!😳😳😳😳. Anawakilisha kina nani sasa ?? Kina mama au...... Subirini slaa na zito waanze kutuambia ukweli jinsi mlivyouza chama kwa mafisadi na kubadilisha rangi ya kadi kwa shinikizo la freemson. Hapa kazi tu, matumaini peleka angaza.

Anonymous said...

Kweli mdau wa kwanza wamekuparura inabidi ukaogee maji ya mruturutu