ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

Albino avamiwa na kujeruhiwa Kenya

Image captionAlbino kama huyu wamekuwa wakilengwa nchini Tanzania

Watu wasiojulikana wanaripotiwa kujaribu kukata sehemu za mwili za mwanamme mmoja mwenye ulemavu wa ngozi au albino nchini kenya, kisa ambacho kimezua hali ya wasiwasi kuwa huenda albino wakalengwa hasa kutoka nchini Tanzania.
Akiongea na gazeti moja nchini Kenya, Enock Jamenya mwenye umri wa miaka 56, alisema kuwa watu watatu walimvamia nyumbani kwake katika wilaya ya vihiga magharibi mwa kenya, ambapo walimuitisha pesa.

Alipowambia hana pesa za kuwapa watu hao walimuomba sikio au mkono wake ili wapate kuuza nchini Tanzania.Viungo vya albino hutumiwa kufanyia uchawi

Kulingana na gazeti hilo , watu hao walijaribu kumkata sikio ,mkono na vidole na kisha wakakimbia na kumuacha Jamenya akiwa na majeraha mabaya.

Katika nchi jirani ya Tanzania baadhi ya wanasiasa wamelaumiwa kwa kununua viungo vya albino ili kutumia kufanyia uchawi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu , yameonya kwa kuna hatari ya kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya albino nchini Tanzania wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Takrian albino 76 wameuawa nchini Tanzania tangu mwaka 2000, huku sehemu zao za mwili zikiuzwa kwa dola 600 na mwili mzima ukiuzwa na kwa dola 75,000 kwa mujibu wa wataalamu wa umoja wa mataifa.
Source:BBC

No comments: