ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 19, 2015

HABARI24 TV--MGOGORO WA NCCR MAGEUZI-MBOWE


Mh MBOWE akizngumza na wahabari mapema leo Jijini Dar es salaam
Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umeitaka Tume ya taifa ya uchaguzi kutoa tamko kuhusu kauli iliyotoleawa na mmoja wa viongozi wa CCM kuwa chama hicho hakipo tayari kuondoka ikulu hata kama kitashindwa katika uchaguzi ujao mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa katika kampeni za Urais mkoani kigoma na mmoja kati ya viongozi wa chama hicho ndugu ABDALA BULEMBO ambapo alisema kuwa hakuna njia inayoweza kuwaondoa ikulu na chama cha mapinduzi hakiwezi kuachia IKULU kwa njia yoyote kauli ambayo imeanza kuibua mijadala mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumza na wanahabari mchana wa leo mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA ndugu FREMAN MBOWE amesema kuwa kauli hiyo imewashtua sana wao kama vyama vya upinzani na kuanza kuwa na wasiwasi kama uchaguzi huo utakuwa na amani kwa kuwa chama chenye serikali kimeapa kufanya njia yoyote ili tu kisiachie ikuluMh MBOWE amesema kuwa kauli hiyo inaweza kuchukuliwa kawaida lakini ni kauli nzito na yenye mafumbo makubwa ambayo yanaweza kusababisha vurugu kubwa na hadi sasa hakuna mtu yoyote wa chama hicho wala tume ya uchaguzi aliyejitokeza kutolea ufafanuzi kauli hiyo.
Amesema kuwa kama kauli hiyo ni kauli ya chama cha mapinduzi ni ukweli kuwa vyama vya upinzani havitaweza kuwa na imani na uchaguzi huo kwa kuwa tayari chama tawala kimesema hakiko tayari kuachia ikulu huku akienda mbali na kusema kuwa kwa kauli hizo hakuna haja ya kuendelea kuwa na uchaguzi ambao chama tawala kinangangania ikulu
Mh MBOWE amesema sasa UKAWA unaitaka tume ya taifa ya uchaguzi kukitaka chama cha mapinduzi kutolea ufafanuzi kauli hiyo kwani kama ndio kauli yao watangaze kabisa kuwa hakuna uchaguzi kwa kuwa utakuwa ni upotevu wa rasilimali za taifa wakati tayari chama tawala hakiko tayari kukubali matokeo..
MGOGORO WA NCCR MAGEUZI.
Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa chadema amesma kuwa sakata linaloendelea ndani ya chama cha NCCR MAGEUZI ni mwendelezo wa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo kuendelea kufika bei ya kutaka kuisaliti ukawa na hakuna lingine.
Hivi juzi viongozi kadhaa wa chama cha NCCR waliibuka na kudai kuwa chama chao kimekuwa kikiyumba kutokana na mwenyekiti wao kufanya kazi za chadema kuliko za chama huku wakidai kuwa wamekosa majimbo mengi ambayo walikuwa wanayatarajia ambapo Mh mbowe amesema kuwa hiyo sio hoja kwani lengo la UKAWA sio chama kuwa na majimbo mangapi bali ni kuhakikisha kuwa wanaibuka na majimbo mengi bila kujali vyama vyao.
Mh mbowe amesema kuwa swala la mgawanyo wa vyama lilienda sambamba na kuangalia uwezo wa chama husika katika jimbo na kusimamisha mtu ambaye anakubalika katika eneo husika ili kuweza kupata ushindi katika majimbo mengi na sio kutoa majimbo hata kwa watu ambao hawakubaliki katika majimbo hayo.
MPANGO WA KUMSHAMBULIA MBATIA
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameibua swala ambalo amesema kuwa wamelipata kuwa kuna mipango ya vijana kutoka chama cha mapinduzi kujifanya ni vijana wa CHADEMA na kumpiga Mbatia wakidai kuwa hawamtaki katika chama hicho jambo ambalo amesema ni mipango mfu kwani tayari chama hicho kimezipata.
Mh mbowe amesema kuwa mipango kama hiyo imekuwa ikipangwa na chama cha mapinduzi na na imekuwa wazi na wamekuwa wakiripoti sana kwenye vyombo vya dola lakini kumekuwa hakuna msaada wowote wanaoupata lakini wamejipanga kiulinzi kwa viongozi wao wote na wanahakikisha kuwa wanakua salama salimini.
MBOWE KUTOROKA NCHI
Akizungumza huku akicheka kwa mshangao mkubwa Mh MBOWE amesema kuwa kuna baadhi ya propaganda ambazo zimekuwa zikienezwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi na maadui wa UKAWA kuwa yeye ameikimbia nchi na haonekani katika kampeni za Mh LOWASA ambapo amesema kuwa ni utaratibu wa kupokezana kazi na sasa Ilikuwa zamu ya MH LISSU na baadae atapokea Mh WENJE ili kupeana nafasi za kufanya kazi za majimbo yao.
Mh mbowe amesema kuwa kuna baadhi ya jumbe za kutengeneza za EMAIL zikimuonyesha MBOWE akiwasiliana na Dk SLAA ambapo amesem ni uongo uliotukuka na hajawahi kufanya hivyo na hajatoka nje ya Tanzania kwenda popote kama wanavyosema huku akisema kuwa kuzushwa kwa mambo hayo ni kutokana na wapinzani wao kuishiwa sera na kuanza kuwadanganya watanzania.

6 comments:

Anonymous said...

CCM haiondoki kweli nyie wenyewe na miungniko wa vyama vurugu mtido mmoja tukiwapa nchi si ndio mtatuumiza saidi boea zimwi likujualo halikuli likakwisha kazi matusi na kuwaita watu wana akili za mgando najua mtakao soma hapa lazima mtukane ila sijali naongea mimi kama mimi CCM MBOVU ILA MAGUFULI SIO MBOVU HAPA KAZI TUUUU,,,,,UKAWA MTASUBIRI SANA KUINGIA IKULU MMEBUGY KUMUWEKA LOWASA,,,,,watanzania wengi wanataka mabadiliko kwa vile wameichoka ccm ila kwa LOWASA hakuna mabadiliko AIWEKE WAZI RICHMOND kama kweli hausiki FISADI papa kugeuka kuwa msafi kwa CHADEMA KISA ILULU HIYO NI BIG NOOOOOO

Anonymous said...

Mh. Mbowe, asante sana kwa taarifa zilizo na uhakika. Zote hizi ni njama ambazo zimeandaliwa na wapinzani wasiotaka wala kukubali kutoka kwenye madaraka ili basi wawalaghai waTanzania na kukosa imani katika kipindi hiki muhimu kwa taifa na bado watakuja na mbinu nyingi sana kwenda mwishoni hivyo Wapenda Amani na Tanznaia ikiwa kwanza then siasa. Hawa wataivuruga sana kameni ila la msingi ni kuwa macho na kulinda kile kinachotakiwa. Wanaoishi kule Amerika wameshangaa kusikia kuwa uko Amerika kitu ambachoo hakipo kabisa na sijui huyo aliyetumw alikuwa mjasiri kiasi gani kuueleza umma kuwa umekutana na Slaa!1 ajabu.!! Chama na tume ya uchaguzi turejesheeni majibu ili kampeni ziweze kuendelea kwa amani. Kumekuwa na mbinu nyingi sana za kuwanunua vijana wa chama tawala kufanya mambo na baadae kudaiwa ni CDM, Ukweli lazima usemwe na tusijeleta machafuko kwa jamii. waTanzania wamejianda, wametulia majumbani, wnahudhuria kampeni kwa amani wakitunza vichinjio vyao tayari kwa siku ya tarehe 25 Okctoba na tunaimani kabisa kutakuwepo na umeme wiki nzima ya kuanzia uchaguzi hadi kutangazwa wasifu. Tunaomba vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema iwezekanavyoo na kukiwa na vifaa vyote husika kwani maandalizi haya ni ya muda mrefu. Mungu ibariki Tanzania na watu wake na vyama vyao.

Unknown said...

Wewe mbowe muongo kuhusiana na kauli yako kwamba CCM wamesema hata wakishindwa hawatoki ikulu. Mbowe kama mwenyekiti wa chama unafahamu taratibu za chama . Kwani Bulembo yeye kama nani ndani ya CCM? Je Bulembo ni mwenyekiti wa CCM? Ni Katibu mkuu wa CCM? Ni msemaji mkuu wa CCM? Ni mwanasheria mkuu wa CCM? Je Bulembo ni mgombea wa uraisi CCM? Kama Bulembo atakuwa hashikilii nafasi yeyote zilizopo hapo juu vipi leo kauli yake iwe ndio kauli ya chama cha mapinduzi? Mbowe waeleze tu watanzania kuwa mambo ya kuingia ikulu kwa upande wa ukawa yanawaendea vibaya kinyume na matarjio yenu na mmeshakata tamaa kuliko kuanza kutafuta visingizio visivyokuwa na mshiko. Usianze kuwatia hofu watanzania kwa kisingizio cha kuzulumiwa na CCM wakati kila mtu anaona uchapa kazi wa magufuli kwenye kampeni zake. Tafadhali acha kauli za kisanii zenye lengo la kuliingiza Taifa katika fitna. Wewe kama mwenyekiti wa chama kabla ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari ulijaribu kumpigia simu mwenyekiti nwenzako au msaidizi wake kulizungumzia suala unalolilalamikia kwa sababu hivyo ndivyo wanavyofanya waliotutangukia katika kuendesha siasa za kistaarabu ? Kwa sababu suala la amani la taifa si jukumu la CCM tu ni la kila la mtanzania. Usisubiri mpaka mtu amwage petroli ili wewe upate sababu ya kurusha njiti ya kibiriti. Watanzania wanajua nyinyi watu wa upinzani si wazendo wa kweli uzalendo wenu upo kunako kitu na hicho ni kuhakikisha mnaingia ikulu kwa harama yeyote zikiwa za udanganyifu, ulaghi au hata kwa vurugu . Naamini tutakubaliana siku zote itakuwa Tanzania kwanza.

Anonymous said...

Mbowe acha kutafuta huruma kwa wananchi kwa kuweka allegations za kupika.Tuhuma za kupanga mauaji au njama za kudhuru kiongozi wa chama haiwezi kuishia kwenye podiums, kama mnaushahidi peleka hao watu mahakamani laa sivyo myamaze mshughulikie issue za wanachama wa vyama vinavyounda Ukawa waliobaini mbinu za Chadema kuwa marginalized.Kuongelea issue za CCM ni janja ya kukwepa issue at stake.Na wachawi hapa ni viongozi wa Ukawa kuweka personal interests ahead of their party's.

Anonymous said...

Kumbe unajua CCM ni mbovu sasa ya nini? Tatizo lanwa Tanzania sio Magufuli wala EL ni Chama kibovu na walaji rushwa wamejaa humo?!! Baasi.

Anonymous said...

Pamoja na ubovu wa CCM bado ule usemi wa "zimwi likujualo halikuli likakumaliza" kwani angalau Watanzania wengi wapenda ukweli wameona na wanaendelea kuona yale ambayo serikali chini ya utawala wa chama hiki imeyafanya. Pamoja na haya CCM imeamua kuyavalia njuga na kuanza kuyashughulikia yale yote wananchi wamekuwa wanayalalamikia ndiyo maana wakamchagua mgombea urais Magufuli ambaye ni mwadilifu, mchapakazi na siyo fisadi kama Lowassa wa Ukawa. Hivyo usilinganishe kati ya Magufuli na Lowassa katika azma hii. Pili, usilinganishe ubovu wa CCM na ubovu wa Ukawa. Wakati CCM wameonyesha dhamira na umaihili wao katika kushughulikia matatizo ndani ya chama, Ukawa ndiyo sasa wamechachamaa kuonyesha jinsi walivyo wabovu, wasivyo na umoja wala matumaini. Vurugu zinazoendelea sasa ndani ya Ukawa ni ishara tosha kwa wananchi kukiogopa kikundi hiki.