ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 25, 2015

Kauli ya Ukawa kususia uchaguzi yaishtua Nec.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeshtushwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kwamba watasusia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hata hivyo, Nec imetetea kauli iliyotolewa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Mgombea urais ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, kwamba CCM haitakubali kuiachia Ikulu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alisema kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi wa chama kikubwa iliwashtua na kwamba katika vipindi vyote vya uchaguzi vilivyopita, hawajawahi kukumbana nayo. Hata hivyo, Jaji Lubuva alisema baada Nec kufuatilia, ilibaini kuwa kilichosemwa na Bulembo, hakiendani na kauli iliyotolewa na Mbowe.

Jaji Lubuva alisema kauli iliyotolewa na Mbowe si tu kwamba inashtua, lakini ni hatari kutolewa katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi ambacho Watanzania na nchi nyingine, zinaamini kwamba uchaguzi utafanyika katika hali ya amani na utulivu. Lakini alisema baada ya kufuatilia, wamebaini kuwa kauli iliyotolewa na Bulembo katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Kigoma ilikuwa ni ya kisiasa na si vinginevyo.

“Bulembo katika kauli yake hajasema kwamba hata kama Nec ikitangaza matokeo CCM wakiwa wameshindwa, hawatakuwa tayari kuwaachia Ikulu Chadema. Alikuwa anamaanisha kuwa watawashawishi wapiga kura wao wasiwapigie kura ili wasipate nafasi ya kwenda Ikulu,” alisema. Alisema kauli iliyotolewa na Mbowe na Bulembo zinakinzana na kwamba baada ya kufuatilia walizinukuu.

“Kukataa matokeo ya uchaguzi hata kama umeshindwa kihalali ni uhaini,” alisema Jani Lubuva.

“Hii ni kauli ya kisiasa kama ambavyo Chadema nao wamekuwa wakitamka kwamba hii ndiyo awamu ya mwisho kwa CCM kukaa madarakani,” alisema Lubuva.

Kadhalika, Jaji Lubuva alikemea na kulaani kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na wagombea, viongozi wa vyama vya siasa na makada wake katika kampeni zinazoendelea kote nchini.
CHANZO: NIPASHE

7 comments:

Anonymous said...

Asante kwa kauli za mkingano. Mimi siko kwa chama chochote bado umri ukitimu nitajiunga kinachoelekea.Niseme tu kwa ujumla siasa za kampeni ninazosoma kwenye magazeti na kuona mwenyewe na kauli za wagombea hasa vyama vikubwa. Tatizo sio mgombea wala kikubwa hapa shida ni chama!! Kwa muda mrefu naona ahadi kibao zikishushwa kuleta maendeleo wakati ile hali ya kulindana haijaondoka!! Vijiji vingi bado ni shidamiundo mbinu, tumeona kipindupindu kinavyosambaa sasa hivi. Kweli wizara husika na wananchi mtaa kwa mtaa kufanya usafi na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi! Huu ni mzaha! Tumeona ume ya uchaguzi kunadilishwa wafanyakazi hivi majuzi kwa mamlaka hii ni kiashiria wazi kabisa cha kutafuta magoli ya mkono. Tunaelekea wapi?? Mungu bariki.

Anonymous said...

Ukawa wanatakiwa kutilia waache mihemko ya kipuuzi sio kupanic . Mara nyingi vyama vya upizani barani Africa vimekuwa vikitumia ticket ya kasusia uchaguzi baada ya kubaini kuwa havina nafasi ya kushinda na hii mara kwa mara imepelekea kuziingiza nchi nyingi barani Africa katika migogoro ya kisiasa isio na ulazimu. Kutafuta sababu za kijinga ili kususia uchaguzi ni dalili tosha kabisa kwamba ukawa wamesha fulia mwaka huu kilichobaki kwa ukawa ni kueneza chuki miongoni mwa wanachi ili kuliingiza taifa katika machafuko ya kisiasa.

Anonymous said...

wee kege ngedere yaani ukawa mwaka huu 2015 haina nafasi ya ushindi.umefyatuka kama nguruwe-mwitu.hivi kweli wewe ni raia wa tanzania,huoni,hupimi trends,husikii,huambiwi.you are real a bastard.unaonaje kama huna hoja zenye mashiko ukakaa kimya,maana kukaa kimya nako ni hekima kuliko kuropoka ukaletea watu kukerekwa.muliobaki na imani za ki-ccm-ccm sasa hivi hamjai mkono,sijui unaniilewa.print hii clip,hifadhi,utakuja isoma tena baada ya uchaguzi mkuu.lowassa hakamatiki,ukawa haikamatiki,seif hakamatiki,ushidi wa kipigo cha mbwa-koko kinawasubiria ccm.

Anonymous said...

Ukawa wameona kina cha maji ni kirefu na kujua kuwa kuogelea na kuvuka ni kazi ngumu hivyo wanataka kudanganya wananchi kuwa wanaonewa ili iwe ndiyo kisingizio chao cha kutaka kujiondoa. Waswahili wanasema “mtoto akililia wembe mpe ..”Kama kweli wamepania kutoka, wacha watoke lakini wajue kuwa hasara ni kwao. Kutoka kwao kutawasaidia wananchi kuwaelewa vizuri kama ni wana siasa wa aina gani na kama wataendelea kuwepo kwenye ulingo huu wa kisiasa miaka ijayo wapiga kura watakuwa na kazi rahisi ya kuamua ikiwa watataka tena kuwaomba kura zao kwani watakuwa wamewaelewa zaidi. Hii ni aibu, kwani asiye kubali kushindwa si mshindani na kama kila chama kitakacho kuwa kinaingia kwenye uchaguzi lengo lake litakuwa ni lazima kushinda basi itakuwa vurumai tupu.

Chama kuweza kukoga mioyo ya wapiga kura na hatimaye kushinda lazima kiwe kimejiandaa vizuri kiutawala, kifedha, kimazingira na san asana kiwe na sera nzuri itakayo wafanya wapiga kura wavutike. Chama kistegemee kuwa wananchi watakibeba tu kwa ajili kina ajenda moja tu ya kutaka kukiondoa madarakani chama tawala. Hilo haliwezekani kwani wananchi watataka kujua chama hicho kitawanufaisha vipi hata kama baada ya kukiondoa chama tawala.

Bado Ukawa wana nafasi nzuri tu ya kujirekebisha pale wanapoona kuna upungufu kwani bado muda upo. Hivi juzi tu wameanza kuchangisha hela kwa ajili ya kugharamia kampeni kutoka kwa wanachama wao na wananchi wengine kama wataamua kujitoa watawaambia nini wafadhili wao hao! Ni maoni yangu kuwa Ukawa muwe wavumilivu na muendelee na kampeni zenu mpaka mwisho na msubiri siku ikifika wananchi wapige piga kura zao kumchagua nani ataliendesha gurudumu la maendeleo ya nchi yetu kwa kipindi kijacho. Wakati huo huo bado mkumbuke kuwa panapo mashindano kuna mshindi na mshinde. Lolote lile litakalo kuwa baada ya uchaguzi bado nchi inahitaji ushiriki wa vyama vya upinzani kwani hii ndiyo njia pekee ya kuendeleza kujenga demokrasia nchini kwetu.

Anonymous said...

Pipoziiiiii powerrrrrrr kila siku wao tu hebu pigeni kinya basiiii,,,,,,si mshajipanga kuingia ikulu subiri mwezi wa 10,,,,,,

Anonymous said...

Usibane baadhi ya mitundiko; be fair and reliable!

Anonymous said...

CCM Oyeee!!!!!!!!!!!