ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 22, 2015

LOWASSA ALIVYOFUNGA KAZI MASASI, MKOANI MTWARA LEO

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara, kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea nafasi, uliofanyika leo Septemba 22, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MASASI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 22, 2015.
Uwanja wa Boma mjini Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani hapo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi (kulia), Mama Modesta Makaidi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Chademaaaaaa.........
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.
Mgombea wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara leo Septemba 22, 2015.

Magambo yenye jumbe mbali mbali.
Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Mmoja wa Wazee wa Mji wa Masasi, akiendeleo kuchukua taswira kupitia simu yake, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
































13 comments:

Anonymous said...

MKUTANO WA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA ZAKHEM-MBAGALA UMATI WA KUTISHA TULIKUWA MILLION 2.HII ILIKUA NI JUMAPILI TAREHE 20 SEPTEMBA 2015,MKUTANO WA MHESHIMIWA LOWASSA UWANJA UMOJA MTWARA JUMATATU TAREHE 21 SEPTEMBA 2015 UMATI ULIKUA NI MILLION 2,WATU KUMI WALIZIMIA,LEO HII UWANJA WA BOMA MASASI UMATI WA WATU ULIKUA NI MILLION 2.2 UMEZIDI ULE WA ZAKHEM-MBAGALA KWA WATU LAKI MBILI.YAANI UTITILI WA MASASI UNGEMTISHA HATA BARACK OBAMA NA GEORGE BUSH KWA PAMOJA.HEBU REJEA KUWAANGALIA SURA ZA HUU UMATI ULIVYOHAMASIKA NA WALIVYO TAYARI KWA LOLOTE LILE. CCM ACHENI MCHEZO, CCM ACHENI CHOKOCHOKO, CCM ACHENI FIKARA CHAFU ZA MIPANGO YA KUIBA KURA HAWA WATU KWA MAMILLION YAO NI WAFUASI WATIIFU WA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA RAIS ANGOJEAYE KUAPISHWA TAREHE ITAKAYOPANGWA BAINA YA PROTOKALI MPYA YA IKULU,UKAWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA HII NI BAADA YA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU WA TAREHE 25 OCTOBA 2015 KWA ZAIDI YA ASILIMIA 80.MASHUJAA WA MASASI TANZANIA YOTE TUNAWAPENDA MNO.

Anonymous said...

I approve this message

Anonymous said...

Asanteni wana Masasi tuko pamoja mimi nikiwa mwana Masasi niko nje ya Masasi ninakubali na nasema tuko pamoja kazi ni moja tuu tarehe 25 mwezi wa kumi ukiwa umetunza kichinjio chako pata kifungua kinywa mapema kumi na moja asubuhi wahi kituoni tumbukiza alama yako ya vyema kwa mh. LOWASA na mbunge wako chama kitokanacho na UKAWA nenda kapumzike nyumbani waachieni mawakala waendelee kulinda haki yako na mawakala wote kuweni na tochi zenye mwanga mkali kukwepa wazushi wakuzima taa na kupenyeza kura feki. AMANI IWE KWA wapenda maendeleo na mabadiliko. Utawala wa chama hiki umetuyeyusha waTanzania. Escrow wamegawana hatutaki kuwapa waendelee kutunyonya. Mh. JPM, TATIZO SIO WEWE TATIZO NI SERIKALI YA ccm NA MBUNGE Alisema wazi bungeni hivyo haturudi nyuma, njoo upande huu, uliokuw aunagombe nao wengi umewaona wako kimya sana pamoja na kuteuliwa kwenye kamati ya ushindi wanaogopa machafu yaliyotendeka kulindana. !!

Anonymous said...

Wakati ukitaka kuandika uongo hebu jaribu kufikiria kwanza halafu uchague swala ambalo litakuwa gumu kwa watu kulipinga. Pamoja na mawazo yako kuwa Watanzania ni wepesi wa kuamini jambo, ukweli ni kuwa bado ni watu makini na wanaelewa sana mambo mengi kuhus nchi yetu. Hivi ukitueleza kuwa watu milioni 2.2 walihudhuria mkutano wenu katika Uwanja wa Boma huko Masasi ni nani unaemdanganya. Kama hujui idadi ya watu wanaoishi Masasi na vitongoji vyake fungua vitabu vyenye takwimu ya watu nchini ili ujielimishe.

Anonymous said...

masasi kidedea,masasi kamili-gado.kumbukeni mtindo wetu ule=ule goli tatu bila.diwani ukawa,mbunge ukawa na urais ukawa yaani mheshimiwa edward lowassa.hii ya masasi ni kiboko,alibaki kweli mtoto nyumbani?siwaulizi wazee maana wazee wooote wa masasi walikuwepo.hii ni kali,tena kali kweli kweli.

Anonymous said...

Tatizo ni kwamba umati mkubwa umejaa watoto wadogo na vijana ambao hawajafikia umri wa kupiga kura. Kuna tofauti kati ya mashabiki na wapiga kura. Hivyo basi, hapo Oktoba 25, 2015 umati huu wa Masasi na mikoa mingi ambayo Lowasa anao mashabiki hautamaanisha lolote. At the end, CCM itaibuka kuwa mshindi kwa sababu inayowapiga kura wengi.

Anonymous said...

Danganywa na hayo mafuriko. Mbona hata CCM wanajaza watu? Mkishindwa mtaanza kusema mmeibiwa. Mikutano yote ya Kampeni ya CCM na Chadema watu wanajaa. Usidanganyike na hayo mafuriko nenda kapige kura.

Anonymous said...

Tofauti ya mikutano ya ccm watu wanajaa kumuangalia diamond na king kiba wakati ukawa watu wanajaa kusikiliza sera za wagombea. Fiesta oyee.

Anonymous said...

Mimi ni CCM damu and I can honestly say EL na hii mikutano yake makes me nervous. Naomba tutafute muarobaini wa huyu jamaa kwani sera zetu nyepesi za kusema watu wanapewa hela kuudhuria mikutano yake haziuzi jamani. Vinginevyo tusije aibika October 25.

Anonymous said...

Mafuriko ya nini? Watu wanafurika ili kusikiliza kile mgombea atakachoenda kutekeleza (sera).Sasa haya mafuriko ya kutafakari sura ya mgombea! The guy cannot talk!

FREEDOM OF PRESS said...

Kwani hao wanaokuja, CCM chama cha Mafisadi, wamejiandikisha, wote?

Anonymous said...

UWWIIIII, WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO, LICHA YA SLAA, NA LIPUMBOA KUUNANGA UKAWA WAPI, CCM MJIANGALIE, MNATOA AHADI SANA, MKIPITA MNABORONGA, HALI ZA MAISHA ZINAKUWA NGUMU, WATU WAMEWACHOKAAAA.

Anonymous said...

Nyinyi sherehekeni tu wakati huu itakapofika 10/25 ndiyo mwisho wenu. Sisi na mwendo wetu wa kusuasua tutajitokeza kidedea kwani wasemaji walisema "mwenda pole hajikwai"!