ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 28, 2015

MAELFU WAMPOKEA EDWARD LOWASSA JIMBO LA BUMBULI MKOANI TANGA

Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
 Lowassa akiwasili Bumbuli.
 Lowassa akihutubia mkutano wa kampeni jimbo la Bumbuli leo.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba 28, 2015.

4 comments:

Anonymous said...

Lowassa mwaga sera na ahadi
Matusi na kashfa vijembe waachie wao

Anonymous said...

tunakushukuru mheshimiwa lowassa kwa kututembelea jimbo hili la bumbuli,karibu sana rais wetu mtarajiwa wa awamu tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania.mapokezi haya makubwa mno uliyoyapata leo ni ishara ya wazi kuwa wananchi wengi wa jimbo la bumbuli wapo tayari kwa mabadiriko na tunasafiri na wewe pamoja katika safari ya matumaini.umati huu uliyokupokea haujawahi kutokea katika jimbo hili tangu tupate uhuru miaka 55 iliyopita.jimboni hapa zipo famili mbili zenye ujeuri mkubwa wa pesa na matumizi ya hila chafu za kujitafutia umaarufu na kusujudiwa.ni famili mbili tuu.ya yusuph makamba na ya benjamin mkapa.hawa ni wezi, fedhuri,jeuri,wamejaa kiburi,wanajitahidi kuwapotosha watu,waporaji,majambazi wa kisiasa.hawa wametuibia sana.mheshimiwa mara uingiapo ikulu[ tunauhakika na hilo asilimia mia moja] dola iwamulike wezi hawa na hatua stahiki,tena za haraka zichukuliwe dhidi yao.karibu,karibu.

Anonymous said...

Pole ndugu yangu uliyenitangulia kutoa maoni, kama Unategemea lowassa ataleta maendeleo ya tanzania, Unaota ndoto ya mchana kabisa. Lowassa ni mwizi na fisadi mkubwa, hao wengine hawajawahi kuwajibishwa kwa ajili ya ufisadi, yeye alikubali na akawajiba. Na hajui chochote unachomwambie akikifanye ikulu, maana ye ni hiyo CCM unayoisema, amekuja huko kutaka urais tu na sio kuleta maendeleo yoyote. Na hao walikokuja uwanjani sio wote ukawa, wengine wamekuja kumuona kama kweli ataj.ny.a tena.

Anonymous said...

Ikulu haioni ng'o! Tanzania siyo Bumbuli peke yake hata mkimpa kura zote asilimia 100!