Vijana wanao saidia kuokota mipira katika uwanja wa taifa wakati wa mechi mbalimbali za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zikichezwa, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum unaohusu kuhamasisha Usalama barabarani na kutoa elimu kwa wapenzi wa mpira wa miguu na wachezaji,wakati wa mpambano wa ligi hiyo juzi iliyowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mshambuliaji
wa timu ya Simba,Hassan Mgosi akijaribu kumtoka kiungo wa timu ya Yanga
Harouna Niyonzima wakati wa mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara iliyochezwa
kati ya timu hizo mwishoni mwa wiki katika uwanja wa taifa jijini Dar
es Salaam,Ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
No comments:
Post a Comment