MAGUFULI AMTOSA CHENGE BARIADI.
Katika kile ambacho wachunguzi wa mambo ya kisiasa wamekiita tukio la kimapinduzi na mwanzo wa mabadiliko mapya ndani ya CCM, Mgombea wa Urais kwa ticket ya CCM Dr. John Magufuli amefanya kile ambacho Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa wameshindwa, kumtosa Andrew Chenge hadharani.
Mwanasheria huyo mkuu wa zamani ambaye anahusika kwenye kashfa mbalimbali zilizozikumba taifa hili, ambaye ndio alikuwa mratibu wa kampeni za Urais za Edward Lowassa alipokuwa CCM alijikuta kwenye wakati mgumu leo pale ambapo Dr. Magufuli alipogoma kumpandisha jukwaani na kumkabidhi ilani ya CCM kama anavyofanya kwenye majimbo mengine. Magufuli ambaye mpaka sasa ameweka wazi adhma yake ya kuanzisha Mahakama ya Mafisadi, inasemekana aliweka msimamo wake wazi mbele ya Mwenyekiti wa kampeni za CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwamba hana mpango wa kuwanadi wana CCM wowote ambao wana kashfa za ufisadi, na amepewa baraka zote za kukisafisha Chama cha Mapinduzi ili kuonyesha tofauti na mgombea wa UKAWA ambaye ana kashfa lukuki za ufisadi.
Tukio hili la leo linaelezewa na wachambuzi wa Siasa kama mwanzo mzuri wa Magufuli kujitofautisha na makada wa CCM wasio wasafi na kurejesha imani ya Watanzania kwamba yeye ndio atakayeleta mabadiliko bora zaidi kwa Wananchi.
Itambuliwe pia, Dr. Magufuli amefanya kazi katika awamu zote mbili za Rais Mkapa na Kikwete na hajapata kashfa yoyote, tofauti na mgombea wa UKAWA ambaye kwa kipindi cha miaka 40 aliyokuwa ndani ya CCM amepata kashfa lukuki ikiwemo ya Richmond, Ranchi za serikali, na kwa sasa kuna sintofahamu kubwa kuhusu kauli zake za kuomba kura- kanisani na hali yake ya kiafya.
Kwa sasa Dr. Magufuli amefaulu kizingiti hiki kikubwa cha Mheshimiwa Chenge, na kugoma kwake kumnadi kunatuma ujumbe kwa wale mafisadi wote wa ndani na nje ya chama kujipanga kwani anaonekana ana nia ya dhati kusafisha Chama na Serikali ili kuwapa Watanzania mabadiliko chanya wanayoyahitaji.
HAPA NI KAZI TU.
11 comments:
Baaado saaana hiyo haitoshi kabisa. ccm wako na zaidi ya miaka 54 ya kujisafisha. Bado wako vigogo weeengi sana katika hiyo hiyo ccm ambao anapanda nao jukwaani na kupiga kampeni pamoja na hawawafanyiii kitu. Kama kweli huyu Magufuli ni jasiri basi aanze na hao mabosi wake. Huyo Chenge is just a weakest link. Hebu waache kutudanganya. Kama wewe ni ccm basi wakati wote uko kwenye chama cha mafisadi. KAMWE!!! MABADILIKO HAYATALETWA NA ccm.
Mwandishi ameandika "Magufuli tofauti na Lowassa mwenye tuhuma lukuki za ufisadi"....mi niliachia kusoma hapo
Ujinga mtupu huo. Hii blog naona imeshakuwa mouthpiece ya CCM.
Luke usiwe unaruhusu habari za uongo kwenye blog yako. Huyu jamaa anadanganya umma kwa kusema eti magufuli hana kashfa yoyote na eti chenge ndie alikua coordinator wa campaigns za lowassa. Ebu ifute hii na mwambie jamaa taarifa kama izi huwa zinapelekwaga kwa michuzi.
Hongera sana rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutuonyesha dhahiri yale unayoyasema, tumekukubali, MUNGU akubariki sana. Tumeshuhudia wenyewe kwa macho yetu kuwa huna urafiki na mafisadi, kama ambavyo UKAWA wanavyowakumbatia mafisadi papa, akina Lowassa.
Tunategemea kuona baraza lako lenye waadilifu na wachapakazi wote akina Mwakyembe, Pia tunategemea kuwa na Tanzania yenye viwanda.
Acheni hizo ccm. Jamaa kamkataa kwa vile alikuwa kwenye kamati ya kambi ya Lowassa kule Dodoma. Mbona hakufanya hivyo kwa Sospiter Muhongo ambaye kajiuzuru? Tutaona Kama atafanya hivyo kwa mama Tibaijuka, acheni kuwadanganya wananchi.
Embu, tusifanyane wajinga, na ujanja wenu. Mbona Muhongo kapandishwa Jukwaani na huyo huyo Tingatinga au hakuchukua hela ya Escrow, na Tibaijuka Je? Embu kuweni na haya nyie CCM. na wengine hapo mnawaficha eti mnamuona Chenge tu. Shhh!!!!!!!!!!!!!!
Magufuli kiboko hata Lowasa kakiri kwa kumuita sio mwanamume wa kawaida bali ni dume la ng'ombe . Sasa nyinyi wapambe pigeni kelele huyo mnaempigania yaani lowasa kuwa anafaa anakiri kuwa magufuli ndie anaefaa kuwa raisi sasa msije mkasema lowasa nae kanunuliwa na CCM.
Nyie andikeni mnachotaka kuandika Watanzania watafuata mioyo yao inakowapeleka baada ya kusikiliza hoja, sera na vitendo vya kila mgombea. Uzuri ni kuwa rekodi za hawa wagombeaji nyingi zimeshaanikwa wazi na Watanzania wenye uchungu na nchi yao wameshaziona au kuzisoma. Pamoja na haya yote Watanzania wengi pia tayari wamebaini kuwa kuna wanagombea ambao tayari wameshawadhihilishia kuwa wao ni wachapa kazi na kuna wengine ambao ni maneno mengi tu lakini vitendo vyao haviendani na hayo wayasemayo. Tarehe 25/10 ni tamti ya kila kitu na kila mgombea atachuma alichopanda.
CCM Oyeeee!!!!!
Ccm oyeeeeee
wewe get your fact right, nani alikwambia muhongo alihusika na escrow, muhongo amejiuzulu maana kashfa imehusu wizara yake. huo mgao wa escrow tayari ulikuwa toka mwaka 2006, kabla mahakama haijaamua kusimamisha malipo yake. lowasa ndiye mhusika mkuu, na karamaghi ndiye anayemfadhili kumpa mabilioni. hamumuoni huyo fisadi wenu anayenunuliwa na kina karamaghi na rostam, shame on you!!! muacheni muhongo yeye anajua nini maana ya kiongozi kuwajibika, ukiwa kiongozii mambo yakiharibika hata kama hauhusiki inabidi ujiuzulu kuonyesha ukomavu, sio huo papaa fisadi mpaka raisi kikwete alimlazimisha kujiuzulu la sivyo alikuwa anamfukuza. kwa hiyo hujaandika comment fanya kwanza utafiti wa habari, ukawa utawajua tu kwa bendera fuata upepo, ukiambiwa simama, unasimama, inama unainama bila hata kuuliza. subirini oktoba 25, mtakula sana mandimu
Post a Comment