Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja
wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA.
Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili
hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama
ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali
yake, lakini pia atawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao
hawalipi kodi
Magufuli amewataka Wananchi kumuamini
kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na
kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake
na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za
Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.
Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango yao
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka
kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia Mkutano.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa
Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa
wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika
Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi
ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe
kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni
humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia jambo
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia
wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi
jioni ya leo.
Baadhi
ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia
aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango yao
Kada
maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba
akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia
chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na
kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais
Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Kada
maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba
akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa
Kawawa mkoani Kigoma
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Kawawa mjini Kigoma leo.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (kuliaakifurahia jambo na mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia CCM, Peter Serukamba wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Kawawa mjini Kigoma leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wananchi wa Kigoma wakifurahia hotuba ya Dk Magufuli kwenye mkutano huo.
| Ni furaha tupu kwa wananchi hawa wa Nguruka baada ya kumuona Dk Magufuli |
Moja ya mabango yakielezea kero na kumtaka Dk Magufuli azitafutie ufumbuzi
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kata ya Nguruka Jimbo la Kigoma Kusini
Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli
Mgombea ubunge jimbo la Kigoma Kusini kupitia CCM, Husna Mwilima (kushoto) akizungumza na Mmiliki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka wakati wa mkutano huo.
Wananchi wa Nguruka wakiwa na furaha baada Dk Magufuli kuahidi kutatua kero zao atakaposhinda urais
Dk Magufuli akimkabidhi Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima kitabu cha Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano huo wa kampeni
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema, akionesha magwanda baada ya kuyavua alipotangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Nguruka
Dk Magufuli akiangua kicheko alipokuwa akishuhudia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema, akivua magwanda baada ya kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Nguruka, Kigoma Kusini.
Dk Magufuli akionesha moja kadi za alizopokea kutoka kwa wapinzani walioamua kujiunga na CCM
Dk Magufuli akionesha kadi mbalimbali alizopokea kutoka kwa wapinzania walioamua kuvihama vyama vyao na kutangaza kujiunga ba CCM katika mkutano huo wa kampeni
Dk Magufuli akisaidiana Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima kuzisambaza kadi mbalimbali za wapinzani zilizorudishwa
Dk Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani walioamua kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Nguruka, Kigoma Kusini.
Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli alipozuiwa Eneo la Uvinza wakati msafara wake ukielekea Kigoma mjini
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi eneo la Uvinza mkoani Kigoma
Moja ya mabango yenye ujumbe wa kuwasuta wafuasi wa vyama vya upinzani wanaoshabikia Ukawa
Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, Abdallah Bulembo akitangaza kwa wananchi wasifu wa Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli mjini Kigoma.
Wasanii wa kikundi cha Ze Orijino Komedy wakitumbuiza katika mkutano huo wa kampeni
Akijinadi kwa wananchi mjini Dodoma
Dk Magufuli akiwaaga
Dk Magufuli akiwaaga wananchi baada ya mkutano wa kampeni kumalizka mjini Kigoma leo
Dk Magufuli na viongozi wengine wakicheza muziki baada ya kumalizika kwa mkutano




















7 comments:
Ndugu Luke, hivi vichwa vya habari vinaonyesha wazi kuwa wewe ni mshabiki mkubwa wa CCM. Anyway, ni blogu yako we endelea tu kwani vile vile we si muandishi uliyesomea hii fani
Mke wa Magufuli yuko wapi? Mbona haonekani?
What do you mean "KAMA MFALME"!! u najua waandishi pamoja na kuandika mnapotosha sana habari na kwa namna nyingine ni kushabikia au kushoboka.!! Ukweli wa somo.sio.!!
Kwa kweli hakuna haja ya kumlaumu Dj Luke cha msingi kuwa mvumilivu tu hiyo ndio demokrasi tustahamiliane kesho zamu ya kusifisifiwa unaempenda japokuwa astahili sifa .
Wewe ni mwaminifu na mchapakazi
Mwadilifu, mtulivu na mchapakazi
CCM Oyeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
Post a Comment