ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 16, 2015

MAGUFULI APOKELEWA KAMA MFALME KIGOMA,WANANCHI WAKIRI WAZI ATOSHA KUWA RAIS

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA.
 Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi

Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.

Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango yao
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia Mkutano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia jambo
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi jioni ya leo.
Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango yao
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais

Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Kawawa mjini Kigoma leo.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (kuliaakifurahia jambo na mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia CCM, Peter Serukamba  wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Kawawa mjini Kigoma leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wa Kigoma wakifurahia hotuba ya Dk Magufuli kwenye mkutano huo.
Ni furaha tupu kwa wananchi hawa wa Nguruka baada ya kumuona Dk Magufuli





 Moja ya mabango yakielezea kero  na kumtaka Dk Magufuli azitafutie ufumbuzi
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kata ya Nguruka  Jimbo la Kigoma Kusini
 Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli
 Mgombea ubunge jimbo la Kigoma Kusini kupitia CCM, Husna Mwilima (kushoto) akizungumza na Mmiliki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka wakati wa mkutano huo.
 Wananchi wa Nguruka wakiwa na furaha baada Dk Magufuli kuahidi kutatua kero zao atakaposhinda urais



 Dk Magufuli  akimkabidhi Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima  kitabu cha Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano huo wa kampeni
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema, akionesha magwanda  baada ya kuyavua alipotangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Nguruka
 Dk Magufuli akiangua kicheko alipokuwa akishuhudia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema,  akivua magwanda baada ya kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Nguruka, Kigoma Kusini.
 Dk Magufuli akionesha moja kadi za alizopokea kutoka kwa wapinzani walioamua kujiunga na CCM
 Dk Magufuli akionesha kadi mbalimbali alizopokea kutoka kwa wapinzania walioamua kuvihama vyama vyao na kutangaza kujiunga ba CCM katika mkutano huo wa kampeni
 Dk Magufuli akisaidiana Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima kuzisambaza kadi mbalimbali za wapinzani zilizorudishwa
 Dk Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani walioamua kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Nguruka, Kigoma Kusini.
 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli alipozuiwa Eneo la Uvinza wakati msafara wake ukielekea Kigoma mjini
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi eneo la Uvinza mkoani Kigoma

 Moja ya mabango yenye ujumbe wa kuwasuta wafuasi wa vyama vya upinzani wanaoshabikia Ukawa
 Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, Abdallah Bulembo akitangaza kwa wananchi wasifu wa Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli mjini Kigoma.
 Wasanii wa kikundi cha Ze Orijino Komedy wakitumbuiza katika mkutano huo wa kampeni
 Akijinadi kwa wananchi mjini Dodoma

 Dk Magufuli akiwaaga
 Dk Magufuli akiwaaga wananchi baada ya mkutano wa kampeni kumalizka mjini Kigoma leo

Dk Magufuli na viongozi wengine wakicheza muziki baada ya kumalizika kwa mkutano

7 comments:

Anonymous said...

Ndugu Luke, hivi vichwa vya habari vinaonyesha wazi kuwa wewe ni mshabiki mkubwa wa CCM. Anyway, ni blogu yako we endelea tu kwani vile vile we si muandishi uliyesomea hii fani

Anonymous said...

Mke wa Magufuli yuko wapi? Mbona haonekani?

Anonymous said...

What do you mean "KAMA MFALME"!! u najua waandishi pamoja na kuandika mnapotosha sana habari na kwa namna nyingine ni kushabikia au kushoboka.!! Ukweli wa somo.sio.!!

Anonymous said...

Kwa kweli hakuna haja ya kumlaumu Dj Luke cha msingi kuwa mvumilivu tu hiyo ndio demokrasi tustahamiliane kesho zamu ya kusifisifiwa unaempenda japokuwa astahili sifa .

Anonymous said...

Wewe ni mwaminifu na mchapakazi

Anonymous said...

Mwadilifu, mtulivu na mchapakazi

Anonymous said...

CCM Oyeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!