ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJINI TABORA LEO

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote. 
PICHA NA MICHUZI JR-TABORA

 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
 Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.

 Wananchi wakishangilia .
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Simiyu wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli kuwahutubia akitokea wilayani Nzega mapema leo mchana
 Wafuasi wa chama cha CCM sambamba na wananchi wa Uyui wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
 Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa na Mabango yao ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,wakimpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassani Wakasubi akitoa ufafanuzi mfupi kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Wananchi wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kwenye mkutano wa kampeni za CCM
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitoa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa mji wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mr. Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwakilishi wa Walemavu Ndugu Amon Anastaz Mpanju mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) akizungumza na Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe na Mgombea wa Ubunge jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala (kulia) kabla ya kuhutubia wakazi wa Nzega waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Parking.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Nzega na kuwahakikishia serikali yake itajali wananchi wa kawaida kwa kuwapauhuru wa kufanya bishara,pia atahakikisha maslahi ya watumishi yanaongezwa.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya parking Nzega kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala wakiwapa shangwe wananchi pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala akiwahutubia wananchi wa Nzega kwenye mkutano ulioongozwa na Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega mjini akihutubia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM alihutubia.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Nzega kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa kata ya Ziba wakati akiwa njiani kuelekea Nzega.
Wakazi wa Bukene wakishangilia hotuba za mgombea urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bukene 
Wakazi wa Bukene wakimsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mikono wananchi aqlipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabota.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akipanda jukwaani  katika mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabota
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akisalimiana na Spika wa zamani wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta  baada ya   katika mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabota
 Sehemu ya umati kwenye mkutano wa kampeni za CCM Tabora
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijadiliana  jambo na  mgombea ubunge Jimbo Nzega Vijijini, Hussein Bashe (katikati) na Mgombea ubunge Jimbo la Nzega Vijijini, Dk Khamis Kigangwalah wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Parking mjini Nzega Tabora
 Dk Magufuli akipanda jukwaani kwa kukimbia mjini Nzega leo
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwanadi kwa wananchi  mgombea ubunge Jimbo Nzega Vijijini, Hussein Bashe (kushoto) na Mgombea ubunge Jimbo la Nzega Vijijini, Dk Khamis Kigangwalah wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Parking mjini Nzega Tabora
Dk Magufuli kijinadi kwa wananchi  mjini Nzega leo

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments: