Taswira ya Uwanja wa Kaitabaulivyo kwa sasa.
Nyasi bandia zikiwa zimewekwa pembeni ya Uwanja tayari kwa kutandikwa katika Uwanja huo
Mwakilishi kutoka shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada
ya kukagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandi katika uwanja wa mpira wa
Kaitaba Amewaomba mafundi kuongeza kasi ili ukamilike kwa muda
uliopangwa. Mwakilishi huyo wa FIFA Mhandisi Kelvin Macklain, alitua
Bukoba wiki iliyopita na kukagua hatua kwa hatua uwanja huo na alifika
hapo kukagua hatua za mwisho kabla ya nyansi husika kuanza kutandazwa,
ambazo tayari zipo katika uwanja huo. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Hata hivyo Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba
Malick Tibabimale, alisema kuwa sehemu ya kati ya uwanja itakamilika
ndani ya mwezi mmoja, na timu ya Kagera sugar itaanza kuutumia uwanja
huo baada ya mechi zake nne za mzunguko wa kwanza. Timu ya Kagera Sugar kwa sasa itaendelea kutumia Uwanja wa Musoma kama uwanja wake wa nyumbani katika Ligi kuu ya vodacom iliyoanza kutimua vumbi jumamosi septemba 12, 2015.
Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja huo Pierre De Groote baada ya kuukagua Uwanja huo alisema watamaliza kazi yote mwezi Disemba mwaka huu 2015.Mhandisi Kelvin Macklain Mwakilishi kutoka FIFA akifanya vipimo katika Uwanja wa Kaitaba unaoendelea kujengwa mpaka sasa. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Sehemu ya katikati ya Uwanja wa Kaitaba ambayo itakamilika mwezi huu wa tisa.
Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com
No comments:
Post a Comment