Katika kipindi cha Sept 26, yalifanyika mahojiano na FRANCIA DTR. Mtanzania anayeishi nchini Uingereza.
Kilimanjaro Studio sasa inakuletea kipindi cha muziki wa kizazi kipya kila siku ya Jumamosi saa 4 asubuhi kwa saa za Amerika ya mashariki
Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi ni Buheti Abdulrahman
Kipindi hiki kitakuwezesha kujua mambo yaliyojiri kila wiki kuhusiana na muziki na wanamuziki wa Bongo Flava na nafasi pekee ya kuweza kuburudika na muziki wa Bongo Flava huku ukipata historia ya wanamuziki hao.
Ni kila Jumamosi ndani ya Kilimanjaro Studio kupitia www.vijimamboradio.com, au www.kwanzaproduction.com au www.bordermediagroup.com au kupitia hapa katika Vijimambo Radio kwenye TuneIn app
Kwa Marekani na Canada, unaweza kusikiliza kupitia simu 716-748-0086 kwa saa 24 ama kwenye live show piga 240-454-0093 na kisha *5 kuchangia lolote
No comments:
Post a Comment