Advertisements

Wednesday, September 2, 2015

Makamba Ashangazwa Na HAYA MAGAZETI MATATU KUHUSU Vichwa Vya Habari Kuhusu Lowassa


Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameonesha kushangazwa na mfanano wa vichwa vya habari vya magazeti ya leo kuhusu mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Makamba ambaye ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, ameonesha kurasa za mbele za magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Tanzania Daima zilizokuwa na vichwa vya habari vinavyomnukuu Lowassa akitaka watanzania wasiogope.
Amepost picha za magazeti hayo kwenye twitter na kuhoji kama mfanano huo ni bahati mbaya au imeratibiwa.

6 comments:

Anonymous said...

Makamba unachoshangaa nini ulitakanyaandikwe Makamba au Magufuli. ??

Anonymous said...

Sasa kuna tatizo gani Lowassa akisema "msiopgope" au tuna takiwa "kuogopa"? hivi ni vichwa vya habari na hayo maneno alisema kwenye mkutano sasa wewe Makamba una tatizo na vichwa vya habari? mbona unafanya kutafuta tatizo lisilo kuwepo? ushauri wangu hili taifa halitaki wananchi woga wala viogozi wasio fahamu kazi zao,huu ni wakati mwingine wa utanadawazi"transparency" hauwezi kubadilika kwa sababu kuna sheria za kipuuzi zinatungwa ovyo bila kuangalia wakati tunao kwenda nao.

Hizi ni siasa za vyama vingi hakuna utawala wa vyombo vya habari unao kibeba chama tawala peke yake hilo ndio mlilolizowea miaka yote ya nyuma, sasa basi mjipange kwa vichwa vya habari vya namna hii sio kulalamika ovyo bila sababu za msingi.

wengi hatuitaki ccm na wengi wanaitaka tusilazimishane tutachagua tunachopenda.

mdau.

manzese.

Anonymous said...

Huyu bwana mdogo ametawaliwa na mfume dume,wacha vyombo vya habari vifanye Kazi,mbona uhuru na mzalendo wameandika kuifavor ccm hujaongea?

Anonymous said...

Tatizo lililopo na wizara unayoshughulikia bado ule ukiritimba upo na umimi. Kwani kuna makosa gani yanayojionyesha kwenye haya magazeti. Au ndio tunaanza sheria za mawasiliano ??!Ulitaka yaandikwe Makamba au Mkapa au Makufuli kasema, kaahidi milioni kadhaa! Samia kaahidi kutoboa maji kila kona ya Mkoa wa Dodoma. Makufuli kaahidi kupunguza gharama za ... Na kadhaa hizi ni habari zinazotakiwa kuwafikia wananchibwa Tanzania gazeti linaweza kufika kjiijini lakini TV sio wote wenye nazo tuweke uhuru kwa waandishi pamoja na sheria iliyoanza isilazimishe vitu nje ya utaratibu.. Asante

Anonymous said...

Nashangaa kuona viongozi wetu wanaweweseka. Sasa vichwa vya habari vinasema USIOGOPE sasa mbona huyu waziri anaogopa? Haya Magazeti yangesema Magufuli kasema Msiogope angefurahi wala asingetaharuki. Sisi waelewa tumeyasoma na tumeelewa kwamba hatutakiwi kuogopa either mawazo wala vitendo. Nakushauri utulie tu ndugu maana kama walisema amehonga mapadre, mashekhe, maaskofu, bodaboda, wapenda mabadiliko, hata haya magazeti anaweza kuwa ameyahonga. Tusiogope tusubiri tu october ndiyo mtajua waoga na wenye uthubutu.

Anonymous said...

Wabunge warudi wakapatengeneze la cvyo kuingia ikulu kwa mabavu kutawaua kwanza