
Joseph Mungai akihutubia mkutano wa UKAWA Mafinga
jina langu ni Tom
Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo ambalo lili mnukuu mgombea urais kupitia Ukawa Ndugu Edward Lowassa alipokuwa akihutubia huko Iringa akiwaahidi watanzania elimu ya bure kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu kuanzia January mwakani 2016. Zaidi aliahidi kulipa madai yote ya Walimu na wafanyakazi wengine wa serikali ambapo haya ni mabilioni ya pesa. Huyu mgombea hakufafanua bayana ni njia zipi zitatumika au vyanzo gani vya pesa vya kugharimia yote haya kwa miezi michache iliyobaki kufika January 2016.
Mimi si mshahabiki wa chama chochote ( independent) bali ninapo sikia ahadi ambazo naziona kama haziwezekani kutimizwa hasa ukizingatia muda uliotajwa na huyu mheshimiwa inasikitisha. Naelewa kwamba nia yake ni kuwa rais, sina tatizo na hilo lakini hili la kuahidi elimu bure kuanzia January mwakani linatia shaka. Labda lengo ni kupata kura za wanafunzi na walimu, sina uhakika. Najua kuna nchi ambazo zinatoa elimu ya bure lakini uchunguze hizi nchi zimeanzia wapi na vyanzo vyake vya mapato ya kugharimia elimu ya bure vinatoka wapi. Hata nchi tajiri kama Marekani ukiacha elimu ya msingi elimu siyo bure.
Baadhi ya hizi nchi wananchi wake hutozwa kodi kubwa sana kitu ambacho ni kama haiwezakani kwa Tanzania kwani ajira zenyewe bado ni shida na kilimo ndiyo hivyo tena. Wakati huohuo huyu mheshimiwa anasema ataondoa ushuru wa mazao. ( Hii si ndiyo kodi yenyewe?)
Maoni yangu ni kwamba hawa wagombea ni ama wanajua au wanadhani kuwa uwezo wa watanzania wengi kuelewa mambo au takwimu bado ni mdogo sana ( so they can get away with it) na hii imekuwa kama utamaduni kwamba waambie wanachotaka kusikia nipate ninachotaka mambo mengine baadae.
Juzi hapa Lowassa aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa jangwani kumsikiliza akiahidi kwamba kuna vigogo wengi wa CCM wangejiunga na UKAWA. Labda kama nilipitwa lakini sijasikia hao vigogo wengine wakijiunga na UKAWA angalau siku hiyo ya ufunguzi. Ni jambo dogo lakini kwa mgombea urais inashusha credibility.
Ujumbe kwa wagombea wote, Achaneni na kuongea na watanzania kama mnaongea na watoto. Na watanzania tusishabikie tu bali tuwabane hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu kulingana na ahadi ambazo nyingi zinaonekana kama ni hewa. Awe ni mgombea wa ccm au ukawa nk, watwambie ukweli siyo longolongo. Longolongo imepitwa na wakati.
1. Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo familia yako inamiliki Uingereza. Ukasema ni ya mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu, ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?
2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je kwanini Mwalimu alikukataa?
3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama lakini wanatishiwa. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo? Je kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya ,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa, lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi zaidi. Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu?
Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatupa picha gani wananchi?
6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond, chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililoanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa, ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao yote?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa Umma, una lipi jipya ambalo umelisahau, na sasa utalifanya katika huu urais wako unaougharamia kwa pesa nyingi?
9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona wafugaji bado masikini, na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?
10. Umetoa mchango gani kwenye bunge maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia yakipotoshwa na chama chako?
Reuters
9 comments:
Swali langu kwako Bwana Tom (kama ndio jina lako la kweli, not so sure but) Je, wewe ni Independent au unatumikia ccm? Maswali yako yote yanaelekea wazi kuonyesha kuwa ni ya mashine ya ccm ya kuwasaga wapinzani. Your questions seem to be very biased my friend. Ungekuwa ni independent basi ungeyaweka hayo maswali yako na kuya balance vile vile kwa candidate wako wa ccm bwana Magufuli na ahadi zao za ajabu ajabu zenye zaidi ya miaka 53 bila mafanikio yoyote. Mpaka sasa Tanzania nchi ambayo ingepaswa kuwa tajiri imebakia nchi maskini miaka nenda rudi chini ya utawala wa chama chako cha ccm. Hospitals are poorly equipped and you tell me how comes your ongoing president and other big shots government leaders of your country travel abroad for medical treatments. With all do respect the Founding father, the late President Nyerere passed at a hospital in abroad. Can you answer just these few questions. Bila kusahau elimu na infrastructures. Zaidi ya miaka 53, where's ccm taken this Beautiful country other than in the ditch na bado wako wanawadanganya wananchi. Please give someone else a chance and stop hate, bulling and anger.
unajua kwasababu tumezoea kila kitu hakiwezekani kutokana na ahadi nyingi za ccm ni hewa basi mawazo yetu yamesha ganda we jamaa hiyo elimu bure inawezekana acha kubisha kila kitu unawafanya ccm waendele kutuburuza tu
Fikra potovu tu. Huyu bwana ni ccm tu hatumii hata lugha ya kuonekana mwenye Busara. Kwa hiyo kama madeni ya Waalimu ni Mabilioni isitafutwe njia ya kuanza kuwalipa kisa ni nyingi? Tanzania ina mabilioni ya pesa zinazochezewa tu na ccm yako unayoitete. Sasa hivi ndiyo wanahonga watu kwa kuwagawia wenye shida pesa. Hizi zote ni rushwa na Takukuru bado ni mali yao. Aibu tupu. Tuache utoto watanzania tutazame mbele.
Naunga mkono mtoa maada,kwani hii si karne ya siasa za porojo one need to substantiate ni namna gani ahadi zake zitatekelezeka.
Unaongelea kuyataka mabadiliko kutoka CCM then huwezi kuja na the old style of politics za ahadi hewa,kuwa na bunge linalojadili yasiyotekelezeka etc
Cha kushangaza nipale anapotokea mtu wa kuhoji km mtoa mada watu wanamwandama just because ya mahaba na vyama vyao vya kisiasa.Watanzania inabidi tuamke na tuhoji kila jambo kwani "Lisilo leta maana kwenye kauli kamwe haliwezi kuleta maana kwenye uhalisia".
Maswali gani mkuu unayouliza ya miaka 30 iliyopota. Kuna viongozi wangapi wana miradi na majumba makubwa kupindukia hapa Dar na mikoani. Nyumba nyingi wanazokaa maofisa wa ubalozi zote ni za waTanzania wamewapangisha na unajua wanapata kiasi gani kwa mwezi. Chukua mfano wa Ubalozi mkubwa kama USA ulio na maofisa zaidi ya 100 wmepanga nyumba kama 20 za mtu mmoja hiyo ni hela ndogo au kwa kuwa hawajaja kugombea na huwajui kama wapo hivyo na fedha mlima. Hebu tulizana na kama uliagizwa kwa kitu kidogo basi sio muda wake. Unajua Mh. JK ana gorofa kubwa kiasi gani mtaa wa Mali na Kisutu. Hebu acha utani.
Maswali yako ya miaka 3p.iliyopita hayana msingi wowote. Hivi ni matajiri wangapi wako Tanzania EL si lolote nimkitu kidogo sana. Rugemalila aliyegawa hela za ESCROW amezitoa wapi? Na mbona hata uongozi wa juu ulikalia kimya kama sio mtandao. Nchi inamrzwa wewe unatumwa kuandika kulinda mafisadi kina Sitta. Mabadiliko yaja wewe hama nchi..
Hapa najaribu kumjibu mtoa mada. asilimia kubwa ya hela itakayosaidia kulipa mishahara na kusomesha. Itakuwa ile hela ya msamaha wa kodi which Lowassa hatowaachilia walipa kodi,Pili kodi za TRA baada ya kukupotea kipindi cha CCM Mr Lowassa anahakikisha zinawaletea maendeleo wananchi,Pia ile hela ya mzee wa kuwia pipa inatosha kusomesha bure kila mwaka.sijui umenipata kaka Tom
Tunatambua kuwa nchi hii ina mafisadi wengi, but Rugemalira hajaomba ridhaa ya watanzania kuwa kiongozi mkuu wa nchi.Hivyo ni haki kumfanyia Lowasa vetting ili kubaini ana stand wapi kwenye maadili. .
Wana ccm bwana utawajua tu! Alafu mwana ccm huyu hajiamini eti “mimi sina chama” jiamini bwana ww jarida zima umeiponda na kuzungumzia ahadi za lowasa mbona ujaizungumzia na kutoa kasoro kwenye ahadi za magufuli aliye ahidi atawanunulia laptop waalimu woote wakati chama chake kolishindwa kuwalipa mishahara tu yaani ww unaacha kusema utawawekea mazingira mazuri ya kuishi unasema utawanunulia laptop
Post a Comment