Wakala wa Airtel Money katika maeneo ya Metro Mwanza, Bwana John Hainga akichangia mada wakati wa semina ya mawakala inayowapatia fursa ya kupata mikopo isiyo na dhamana ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa Mawakala
Kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea kuboresha huduma zake kwa wateja hususani wajasiliamali wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala kupata mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao
za mikononi.
Airtel imewakutanisha mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na ukuzaji vipato katika biashara zao.
"Ukosefu wa elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio wengi hapa nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha mapato kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi wa taifa .
Kwa kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya uendeshaji biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora ya uendeshaji biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na dhamana kwa zaidi ya mawakala 20,000 kote nchini Ili kusaidia kukuza biashara za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia upatilkanaji wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda ya ziwa wa Airtel, Bwana Raphael Daudi.
Kwa upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo bwana John Paschal alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma hii ya Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha biashara zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji. Lakini pia mafunzo haya yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara zetu kwa ufanisi zaidi."
Airtel katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa wateja wake imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa mawakala, huduma itakayowawezesha mawakala wa airtel money kote nchini kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi 500,000/
No comments:
Post a Comment