ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 28, 2015

MTUMISHI KANISA KATOLIKI AINGIA KANISANI USIKU, AIBA ANASWA!

Imelda mtema wa GPL

HII kali! Mtumishi mmoja anayetumikia nafasi ya ulinzi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro (St. Peter) lililopo Oysterbay jijini Dar (jina halikufahamika), amenaswa katika chumba cha kuhifadhia chakula kinachoitwa Mwili wa Kristo (ekaristi) ndani ya kanisa hilo.

Kwa mujibu wa mtawa (sista) mmoja wa kanisa hilo aliyeomba hifadhi ya jina, awali tabia ya wizi wa chakula hicho ambacho ni mkate (ekaristi), divai (mvinyo) na vifaa vingine, mali ya kanisa ilikithiri kanisani hapo mpaka kufikia hatua ya baba paroko kuamuru kufungwa kwa kamera ya Closed-Circuit Television (CCTV) ili kuweza kumnasa mwizi huyo.

KUNA WALIOKATWA MISHAHARA

Sista huyo aliendelea kuanika kuwa, kutokana na kuibwa kwa vitu hivyo mara kwa mara, tena vikiwemo na vifaa vya muziki na vitu vingine vya thamani, baadhi ya wafanyakazi walikatwa mishahara yao ili kuwaonesha kuwa, uongozi haukubaliani na wizi huo wa mara kwa mara ambao uliashiria dalili ya uzembe.

PAROKO AENDA HIJA


Akizungumza na paparazi wetu kwa sauti iliyojaa unyenyekevu wa ki-Mungu, sista huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona wizi ndiyo umeongezeka, paroko wa kanisa hilo aliwachukua baadhi ya watumishi, wakiwemo masista wa kanisa hilo na kwenda nao hija maeneo ya Pugu, Dar kwa ajili ya kuomba na kufunga ili waweze kumjua mwizi huyo anayesumbua akili za watu wa Mungu.

“Unajua kanisa lilikuwa halifungwi. Lakini baada ya wizi wa mara kwa mara ikabidi lianze kufungwa. Na baadaye paroko aliamua kuchukua waumini kwenda Pugu sehemu ya kuhiji kwa vile kuna watumishi (Wamisionari wa Kibenediktini) walifia pale (Januari 1889).“Lengo la kwenda kule ni kuomba sana kwa Mungu ili mwizi ajulikane mara moja,” alisema sista huyo.

MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU
Sista aliendelea kusema: “Kweli Mungu mkubwa. Baada ya kuomba na kusali kwa muda, Mungu alijibu. Mwanzoni mwa wiki hii (iliyopita), mwizi wetu alinaswa kirahisi.”

ILIVYOKUWA

Sista huyo alisema kuwa, ilikuwa asubuhi, sista mmoja wa kanisa hilo alifungua mlango na kwenda kwenye chumba cha ekaristi kwa lengo la kuandaa mambo kwa ajili ya misa ya asubuhi.Ilidaiwa kwamba, sista huyo alipoingia katika chumba hicho alishangaa ku

kuta mwanamke (kwa maana ya mavazi na wigi kichwani) amesimama kwenye eneo hilo akionekana kuwa bize.
“Sista alishtuka sana, akatoka nje na kufunga mlango kwa nje na funguo ili aende akawaite watumishi wengine, akiwemo baba paroko lakini alishangaa ‘mwanamke’ huyo naye akifungua mlango kwa ndani na kutoka. Ina maana alikuwa na funguo zake.”

AITIWA MWIZI

“Ilibidi sista aite mwizi kwa sauti ya juu, lakini mwanamke huyo alitaka kukimbia na kuanza kushindana na sista kwa purukushani za hapa na pale, ndipo watu wakatokea na kumweka chini ya ulinzi ili kumhoji zaidi. Lakini muda wote huo, sista huyo alikuwa akijiuliza mbona mlinzi hakuonekana eneo hilo!”

WAMKAGUA, WAKUTANA NA MSHANGAO

Baada ya kuhakikisha hawezi kutimka tena, mwanamke huyo alianza kwa kupekuliwa lengo kubaini kama kuna vitu alivyokwapua ndani lakini katika hali ambayo haikutegemewa, waligundua hakuwa mwanamke, ni mwanaume ‘njemba’, tena ni mlinzi wa kanisa hilo na kwamba alivaa wigi na dela, vitu vya mkewe.

APELEKWA POLISI OYSTERBAY


“Kama unavyojua tena, popote anapokamatwa mtu akidaiwa kuiba, kuna baadhi ya watu watajitokeza ili wampige. Wengine walimtendea yule mtu hivyo lakini baadaye alipelekwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay ambako anashikiliwa,” alisema sista huyo.

No comments: