Image copyrightAFPImage captionPanya walitumiwa kunusa na kutambua yalikokuwa mabomu yaliyotegwa ardhini Msumbiji
Msumbiji imeondoa bomu la mwisho lililotegwa ardhini baada ya juhudi za miongo miwili za kuondoa kabisa mabomu hayo.
Takriban mabomu 171,000 yaliondolewa kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Halo Trust ambalo limekuwa likiongoza juhudi hizo.
Mabomu hayo yalitegwa wakati wa vita vya muda mrefu vya kupigania uhuru wa taifa hilo na wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mabomu hayo yalikuwa yakitegwa hadi miaka ya 1990.
Panya walitumiwa kunusa na kutambua yalikozikwa mabomu hayo.
Shirika la Halo Trust ambalo limetoka Uingereza limesema nchi hiyo ndiyo ya kwanza kati ya nchi zilizojazwa mabomu ya kutegwa ardhini kutangwa kuwa huru kutoka kwa vilipuzi hivyo.
No comments:
Post a Comment