ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 16, 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI DARAJA LA KIKWETE JUU YA MTO MALAGARASI MKOANI KIGOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea Kusini Mhe. Chung II, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Korea Kusini uliojenga Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi mara baada ya kulifungua rasmi Daraja hilo lenye urefu wa mita 275 na barabara unganishi zenye urefu wa Km. 48.
Muonekano wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye uwezo wa kubeba tani 180 na kudumu kwa miaka 100 kama likilindwa na kupitisha mizigo isiyozidi uzito.

2 comments:

Anonymous said...

KWA JINSI TUNAVYOENDELEA TUSIJE SHANGAA HUKO MBELENI KUPAPATA KIONGOZI TAAHIRA MWINGINE MWENYE EGO AMBAYE ATABADILISHA JINA LA NCHI AU MLIMA KILIMANJARO KUWA MAJINA YAKE.

Anonymous said...

Kila ukifikia wakati wa uchaguzi ndo wakati kufungua kila
Tumechoka na hadaa hizi
Kwani rais sasa hana kazi in kufungua tu
Majumba, barabara na kuaga
CCM
Poleni