ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

Waziri mkuu Australia apokonywa uongozi


Image copyrightGettyImage captionAbbott alikuwa amekabiliwa na wakati mgumu uongozini

Australia inaelekea kupata waziri mkuu mpya baada ya Tony Abbott kuondolewa uongozini katika chama cha Liberal na waziri mmoja wa chama chake.

Kwenye uchaguzi wa kiongozi wa chama uliofanywa haraka, Bw Abbott, ambaye umaarufu wake umekuwa ukididimia kwa mujibu wa kura za maoni, alipata kura 44 huku waziri wake Bw Malcolm Turnbull akipata kura 54.
Wabunge wa chama hicho hata hivyo walimpigia kura Julie Bishop kusalia kama naibu kiongozi wa chama hicho.

Bw Turnbull anatarajiwa kuapishwa baada ya Bw Abbott kumwandikia gavana mkuu na kujiuzulu.

Mapema Jumatatu, kwenye kikao na wanahabari Canberra, Bw Turnbull alisema iwapo Bw Abbott angesalia kiongozi wa chama hicho, serikali ya muungano ingeshindwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Alisema ilikuwa vigumu kwake kufanya uamuzi huo, lakini kwamba ni “wazi kuwa serikali haijafanikiwa katika kutoa uongozi wa kiuchumi unaohitajika” na kwamba Australia inahitaji mtindo mpya wa uongozi.

Bw Turnbull atakuwa waziri mkuu wa nne wa Australia tangu 2013.

Waziri mkuu wa chama cha Leba Julia Gillard aliondolewa uongozini na Kevin Rudd kwenye kura ya uongozi wa chama Juni 2013, miezi kadha kabla ya uchaguzi mkuu ambao chama cha Liberal, chake Tony Abbott, kilishinda.

Bi Gillard mwenyewe alikuwa amemuondoa Rudd kama waziri mkuu 2010.

1 comment:

Anonymous said...

This is how it is done. Siyo Bongo kiongozi hata akiwa uozo basi ataendelea tu mpaka 10 years iiishe. Wot a joke!!