Advertisements

Wednesday, September 2, 2015

ZIARA YA SHIRIKA LA KIMAENDELEO PLAN INTERNATIONAL WILAYA YA KISARAWE

4
Meneja wa Plan International Kisarawe kulia William Mtukananje akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa kupinga ukatili kwa watoto unajulikana kwa jina la Violence Against Children (VAC) katika ofisi za paln international Wilaya ya Kissrawe kulia ni Mratibu wa Mradi wa kupinga ukatili kwa watoto kutoka Shirika la Plan International, Neema Daniel
(Picha na Victor Masangu)
1
Mratibu wa Mradi wa kupinga ukatili kwa watoto kutoka Shirika la Plan International, Neema Danielni akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusna na mradi huo wa kupinga ukatili dhidi ya watotoujulikanao kwa jina la Violence Against Children (VAC).

2
Baadhi ya wadau na maafisa wa plan international wakisikiliza kwa umakini katika mkutano huo wakati wa mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.
3
kushoto ni mwandishi wa habari hizi Victor Masangu akifanya mahojiano na mmoja wa wadau walioshiriki katika mkutano huo wenye lengo la kupinga ukatili na unyanaysaji wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la Plan international.

VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
SHIRIKA la kimaendeleo linalojishughulisha na kutoa misaada kwa binadamu Plan International limebaini kuwepo kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wadogo kulawitiwa hali ambayo imeelezwa inachangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana familia zao kutengana au ndoa kuvunjika na kupelekea watoto wengi kukosa malezi bora na kuishi katika mazingira magumu.
Hayo yamebainika baada ya shirika la Plan international kufanya ziara ya kutembelea katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili watoto hao pamoja na kuweka mikakati madhubuti yenye lengo la kuwalindana kuwapatia haki zao za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa mradi Violence Against Children (VAC) ulianzisha kwa ajili ya kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto kutoka shirika la Plan international Wilaya ya Kisarawe Neema Dainel amesema kwamba kwa sasa baada ya kufanya uchunguzi wamegundua baada ya wazazi kutengana watoto hao wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kulelewa na babu au bibi huku wazazi wao wakiwa hawapo.

No comments: