ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 31, 2015

BALOZI WA TANZANIA OTTAWA-CANADA NA MWAKILISHI WA CUBA Mhe. JACK MUGENDI ZOKA AANDAA HAFLA BAADA YA KUWASILISHA HATI ZA UWAKILISH

Tarehe 22 Oktoba, 2015, baada ya Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka kuwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Mhe. Salvador Mesa, Makamu wa Rais wa Cuba, aliandaa hafla fupi aliyowaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Africa nchini Cuba, mabalozi viongozi wa Kanda mbalimbali na baadhi ya viongozi wa serikali ya Cuba.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wanafunzi wa Kitanzania wanosomea Udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine kilichopo Havana.

MATUKIO KATIKA PICHA
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka akitoa hotuba fupi kwa waalikwa (hawapo pichani)wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba. Katikati ni Mama Baloz, Esther Nyanzila Zoka na kulia ni mkalimani. 
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati) akiwa pamoja na mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba. 
Wageni waalikwa, mabalozi wanaowakilisha nchi zao Cuba na viongozi mbalimbali wa serikali ya Cuba wakiwa katika hafla iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka. 
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kutoka kushoto) akibadilishana mawili-matatu na mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.                                                              

Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kutoka kushoto) akiwasikilza mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba. 
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa kwanza kutoka kulia) akiwa pamoja na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana, wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.


Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana, wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Picha ya pamoja. Kutoka kulia ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje wa Cuba anayeshughulikia masuala ya Afrika, Afisa wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bw. Paul James Makelele, mwanafunzi wa Kitanzania anayesomea Udaktari, Cuba, Mangaro Mabusi na mkalimani. 
Picha ya pamoja. Ujumbe wa Mhe. Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana

4 comments:

Anonymous said...

Du! Jamaa anafanana na Rais Mugabe

Anonymous said...

Alikuwa Usalama wa Taifa huyo, usimchezee ni mtumishi makini, muadilifu na mchapa kazi hodari wa miaka mingi. Mwanae naye ni mdiplomasia pale TZ Embassy, Washington, DC-Marekani.

Anonymous said...

Wewe hapo juu wadanganye wasiojua mambo yalivyo. Mtoto wake kapewa hiyo nafasi baada ha kumaliza shule Minnesota hajafanya kazi foreign affairs.
Mtoto wa kawaida wa mkulima hapati kitu ni kupendeleana tuu. Tutaonana SIRARI

Anonymous said...

HUKU NYUMBANI HATUMJUI.YAANI MNAJUANA WENYEWE HUKO HUKO.BALOZI CANADA,TENA ANAPEWA UBALOZI CUBA,KILOMETER 4000 APART.HUO NI MFANO MMOJA WA MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI.CANADA BAKI CANADA, NI NCHI KUBWA SANA NA INA ENDLESS OPPORTUNITIES KWA AJILI YA KUKUZA MAHUSIANO YA KIBIASHARA,KIUCHUMI,KIELIMU,KILIMO,AFYA,MAWASILIANO,HUDUMA ZA MAJI,NA MAMBO MENGINE MENGI,MENGI.TATIZO KUBWA MABALOZI WENGI WA TANZANIA NJE WANATEULIWA KIMPANGO-MPANGO BILA KUFUATA VIGEZO VYA UWEZO,TAALUMA,UZALENDO,UBUNIFU-MAHUSIANO. HAWA LIKIZO ZAO HUBAKI MAJUU,WATOTO WAO SHULE MAJUU,HATA UKIMUULIZA TANZANIA INA MIKOA MINGAPI HAJUI,ANAKUANGALIA USONI.TUBADILIKE WASHIKA DOLA WETU,UNAWAONA WENZETU-KENYA,UGANDA NA RWANDA KWA UCHACHE?NADHANI MAGUFULI ATAWEZA,ATAWACHUJA,MIZIGO WATAREJESHWA NYUMBANI WARUDI MAOFISINI.