Mratibu wa party hiyo, Abdul Ally ‘Mangi
wa Vocha’ akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) kulia kwake ni
mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa Msofe, Kushoto ni mweka hazina wa party hiyo,
Pinnar Sangawe. Waliosimama kuanzia kushoto ni Ismail Mussa mwakilishi wa TMT
mwaka 2015, mwakilishi wa video Queen, Sophia Hassan, Mwakilishi wa Comedy,
Sharo Mahela.
Mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa
Msofe akifafanua jambo.
Wasanii wa
filamu Bongo wanaounda kundi la mtandao wa kijamii la whatsapp linalojulikana
kwa jina la Bongo Talent Swahili wameandaa sherehe ya kundi lao
linalowajumuisha wasanii mbalimbali wa maigizo ambalo linatarajiwa kufanyika
Oktoba 17 mwaka huu katika Hoteli ya KD iliyopo Kijitonyama jijini Dar.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa sherehe hiyo, Abdul Ally ‘Mangi wa Vocha’
alisema kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa na wageni waalikwa ambao ni mastaa
wakubwa wa Bongo muvi, ambao ni Baga Mteme, Faridi Uwezo, John Kallage na
wengine kibao.
Naye
mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa Msofe alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na
burudani za aina mbalimbali, chakula na vinywaji huku suala la muhimu kabisa
likiwa ni kubadilishana mawazo kuhusu mwenendo wa tasnia nzima ya filamu nchini
na kuongeza kuwa party hiyo itaingia hadi mikoani na kuanzia na jiji la Mwanza
ambalo litajumuisha wasanii wa filamu nchini humo.
No comments:
Post a Comment