Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais.
Mwanahabari
Wanahabari
Na:George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kamanda Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi linawataka wananchi wote kurejea majumbani mwao baada ya kupiga kura badala ya kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura kama ambavyo baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wamekuwa wakiwashauri kwa ajili ya kulinda kura.
Alisema Jeshi hilo linapiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote siku hiyo ya uchaguzi na kwamba litawachukulia hatua kali wale wote watakaoonekana kwenda kinyume na agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuvaa sare za vyama vya siasa ama kuonyesha ishara zozote za vya hivyo.
Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP.Ernest Mangu nae ametoa tamko kama hilo akiwataka watanzania kurejea majumbani baada ya zoezi la kupiga kura akisema kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa linaimarisha usalama kwa wananchi watakaokuwa wakitoka majumbani kwenda kupiga kura na kurejea majumbani mwao.
Hata hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam hii leo inatarajia kutoa maamuzi yake juu ya suala hilo la uhalali wa wananchi kubaki umbali wa mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura.
No comments:
Post a Comment