ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 21, 2015

FAMILIA YA DIAAMOND PLATINUMS WAMMWAGA RASMI ZARI THE BOSS LADY


Sasa ni wazi kuwa familia ya staa mkubwa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’ imemtema rasmi mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile wanachodai …. “Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza kuandikaChanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa kina taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini kutokana na kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu ambacho yeye hakiwezi.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho. 
FAMILIA YA DIAMOND HII HAPA
Ili kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu alimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya mkononi, na alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa mambo yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari huko kwao (South Afrika).
“Hata kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu tumegombana wewe yanakuhusu nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia yangu, ninachojua ni kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama Diamond na kukaa kimya huku simu ikiwa hewani. 
Wakati simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika na kujitambulisha kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na habari hizo, kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia. 
Wakati mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko Salum, ghafla tena sauti nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari wetu akaibaini kuwa ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond. 
“Mbona mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo yenu? Nafasi ya Zari imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna msichana mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi tunaruhusiwa kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana naye, lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili mwenzetu. 
“Zari ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia ustaarabu mwingine, tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye kabisa,” alisema Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na namba yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada zaidi zinaendelea kumtafuta

5 comments:

Anonymous said...

Kwani kama kawachosha na uzungu wake nyie inawahusu nini??kama diamond anampenda inatosha ,ndio shida ya familia za uswahilini,hata mkiletewa mwali mswahili hamtakosa cha kusema,pole sana kaka diamond

Anonymous said...

Umatumbi kazi kwelix2.

Unknown said...

kwanza sinilisia kuwa mama dai ananyumba yake?kinachomkalisha hapo kwa mtoto kitugani?sasa mama na watoto wake wasipojirekebisha ,kijana atakuwa anaoa kila siku,huyo mama si ajifunze uzungu? kumbe ndio maana esma aliachika?jifunzeni kuishi na watu tofautitofauti

Anonymous said...

Huyu mama hana bwana natafuta bibi miye
Namtaka sana mama yake Nasibu,

Anonymous said...

Watu wanaenda na teknolojia nyie mtabakia na uswahili wenu tu,kwani inawahusu nini na uzungu wake?khaaa,mnatia na kichefuchefu sasa,badala mfurahi na kumsupport kijana wenu kwa kuwa happy nyie mnaleta za uswahili,inaelekea mnapenda sana kumcontoll diamond,na wewe dada mtu si umeolewa??just have a seat and shut your mouth,