ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 14, 2015

FLORA MBASHA AKIRI: MWANANGU SI WA MBASHA!

Waandishi wetu

OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi.

Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga.

Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu.

“Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema.


“Huyo mwanaume hafai kabisa, ni katili, namfananisha na shetani, anajifanya mwema kwa watu wakati hajawahi kuiomba msamaha familia, sikubaliani kabisa na hukumu ya mahakama, ukweli anaujua kwamba alibaka na hata mkimtaka huyo binti mumhoji nitamleta, isitoshe sasa hivi hata mtoto wake hamjali, hajui anasoma vipi, hajawahi kulipa hata shilingi ya ada, mimi mwenyewe ndo nahangaika kumlea mwanangu Liz ambaye anasoma kidato cha kwanza.

“Hastahili kabisa kuitwa baba sababu mzazi mwenye akili hawezi kutelekeza familia hata kama tumegombana, nimemwachia nyumba niliyojenga kwa pesa yangu na pesa zote aliweka kwenye akaunti yake na zote nilimwachia lakini kashindwa kuihudumia familia.”

Flora anajulikana kuwa na watoto wawili, mdogo akiwa ni yule aliyezaliwa wakati wanandoa hao wakiwa katika mzozo uliosababisha watengane hadi hivi sasa. Alipoulizwa kwa nini anadai aliyekuwa mumewe kumtelekeza mtoto mmoja tu, badala ya wawili, alifunguka.

“Huyu mwanangu mdogo hausiki naye kabisa, tena asiwe anamtaja kabisa kwa sababu hamhusu, hajui hata matumizi yake yakoje, mengine kaka achana nayo tu,” alisema Flora.

Mwimbaji huyo mwenye kipaji alipoulizwa sababu za kufuta kesi ya kudai talaka, aliyoifungua hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati anadai hamtaki na hawezi kurudiana naye, alisema alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na mtu ambaye hata hivyo, alikataa kumtaja.

Flora alisema familia yake haijaridhishwa kabisa na suala la kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili mumewe kumalizika kwa kuachiwa huru na kwamba wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.“Hiyo kesi imeisha kisiasa, Mbasha aliwahi kukiri kuwa ni kweli alifanya kitendo hicho, iweje leo aonekane hana hatia? Tutakwenda kukata rufaa ili haki itendeke.”

Baada ya kuzungumza na Flora, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha kwa lengo la kumuuliza kuhusu madai ya mtoto yule mdogo kutohusika naye kama alivyosema mkewe, naye bila ‘kutafuna maneno’, alisema hata yeye hamtambui huyo mtoto mdogo, ila anaomba arudishiwe mtoto wake mkubwa, Liz na maisha mengine yaendelee.

“Hata mimi simtambui huyo mwingine, ninachoomba anirudishie tu mtoto wangu mkubwa Liz, huyo mwingine sihusiki naye kabisa kama alivyosema, yeye (Flora) ndiye anajua mhusika wa huyo mtoto, lakini si mimi na wala hajakosea kusema hivyo, nililitambua hilo tangu zamani, anipe tu mwanangu wa kwanza,” alisema Mbasha.

Imeandikwa na Brighton Masalu, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya wa GPL

3 comments:

Anonymous said...

Who cares?

Anonymous said...

mpeleke motto kwa gwajima na mchungaji wako mkachunge wazini wenzenu. ulokole gani huo mkop feki kama bidhaa za kichina

Anonymous said...

Wadogo zangu Emmanuel na Flora Mbasha, MUNGU BABA aliyeziumba mbingu na dunia awasaidie sana.

Natumaini hatua mliyofika si kwa akili zenu, ila ni ubilisi anataka kuwavuruga ili jina la BWANA YESU lizaraulike, hivyo msikubali hata kidogo jina la BWANA YESU likatukanwa kwa sababu yenu. Kwa kuwa kuachana si mpango wa MUNGU. Biblia inasema ni kifo tu ndicho kitakachowatenganisha. BWANA YESU anasema isipokuwa kwa ugumu wa mioyo yenu, ndipo mnaweza kutengana.

Ni kweli mengi yamepita katikati ya ndoa yenu, lakini mjifunze kusamehe na kusahau. Neno la MUNGU linasema ili uweze kusamehewa, ni lazima usamehe. Mahali pengine YESU alisema tafuteni kuwa na amani na watu wote, msishupaze shingo.

Biblia ninayosoma inasema, mume ni kichwa cha nyumba. Tena inasema mwanaume mpende mke wako, na mwanamke mtii mume wako( submit yourself to your husband). Nimeshuhudia nyumba nyingi sasahivi kichwa ni mama na sio baba tena.

Ila kuna ibilisi anayetafuna kanisa la MUNGU, kwa nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani, kuna pepo limeibuka kwa jina la haki ya binadamu. Hili pepo ndio linatafuna watu bila huruma. Kwa wenye ndoa, linavunja ndoa za watu bila utaratibu. Na kwa makapera limejiingiza kwa sura ya ushoga. Sasa pepo hilo linanyemelea Tz, ndio maana utaona kila mtu anajihesabia haki na kuanza kutaka talaka na ushoga, kwa kuwa yote haya huenda pamoja. Ukimuuliza anasema anataka kuwa huru kwa kuwa ni haki ya binadamu.

MUNGU atusaidie wote kuyatambua haya. Ninyi wote mmekuwa watumishi kwa kumtukuza MUNGU kwa njia nyimbo, sidhani kama ibilisi anapenda, ndio maana mnachanyikiwa na kuanza kuweweseka, ila BWANA YESU anawapenda sana, angalieni msije mkamsurubisha tena kwa ugumu wa mioyo yenu. Matatizo yote mliyonayo ni madogo sana KWAKE.

Tafadhali ninawasihi kama wadogo zangu katika KRISTO YESU, msijaribu kupeana talaka, rudianeni ili yule mwovu aaibike.

Nawasihi katika JINA LA YESU, mkirudiana ni vizuri kila mmoja akatambua nafasi yake katika ndoa. Tumuombe MUNGU ainue watumishi wake ambao wataweza kueleza bila kutafuna maneno juu ya nafasi ya mke na mume katika ndoa. Haya yakihubiriwa bila kuonea haya mwanaume au mwanamke, ndoa nyingi sana zitapona.

Huko nchi zilizoendelea wanawake wengi sana hata wakibongo wameiga mambo yaliyo kinyume na neno la MUNGU, matokeo yake nao wameingia katika fashion ya talaka. Ukimuuliza anakwambia hii ni ndoa yangu ya tatu au ya nne. Hivi ni kweli watu wameacha kumuabudu MUNGU na wameingia kumuabudu ibilisi ( haki ya binadamu).

Na BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH awabariki sana Emmanuel na Flora Mbasha.

Amina.