ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 29, 2015

HIZI NDIZO SABABU YA KWANINI MATOKEO YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO KURA ZILIZOPIGWA ZANZIBAR HAYAKUATHIRI KURA ZA NEC



Katika uchaguzi wa Zanzibar, utaratibu ni kwamba Watanzania Zanzibar wanapiga kura 5, yaani Rais wa Zanz, Mwakilishi na diwani. Pia wanapiga kura ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge.

Kwenye kituo cha kupigia kura kuna meza 2. Moja ni ya tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) na nyingine ni ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Meza ya NEC ina watumishi wake na Meza ya ZEC ina watumishi wake.

Watumishi wa NEC wanaripoti moja kwa moja kwa NEC na watumishi wa ZEC wanaripoti moja kwa moja kwa ZEC,

Meza ya ZEC inashughulikia uchaguzi wa Rais wa Zanz, Mwakilishi na Diwani na Meza ya NEC inashughulikia uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mbunge,

ZEC wanaongozwa na katiba ya Zanzibar ya 1984 na NEC wanaongozwa na Katiba ya Tanzania ya 1987,

Pia vyama vya siasa wanaweka mawakala wa aina mbili, moja kwenye meza ya NEC na pili kwenye meza ya ZEC,

Hata katika kuhesabu kura hawa watu hawaingilian, ZEC na mawakala wao wanahesabu kura zao na NEC na mawakala wao wanahesabu kura zao.

Pia kuna ballot boxes tofauti. Zipo za ZEC na NEC.

Mzanzibar anapokwenda kupiga kura kwanza anakwenda kwenye meza ya ZEC, anatoa kitambulisho na anapewa kura tatu, Rais wa Zanz, Mwakilishi na Diwani. Anapiga kura na anapakwa wino kidole kimoja.

Baada ya hapo anakwenda kwenye Meza ya NEC anapewa kura 2, Rais wa JMT na Mbunge. Anapiga kura na kuzitumbukiza kwenye mabox ya NEC ambayo ni tofauti na yale ya ZEC.

Wakati wa kuhesabau hawa watu hawaingilini.

Kwa hiyo kasoro katila kura za ZEC, hasa kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura tofauti na wale waliojiandikisha bila kuathili kura za NEC ni kutokana na kuingiliana katila majukumu yao.

Udanganyifu umefanyika kwenye meza ya ZEC ndiyo maana walibaini hizo kasoro walipokuwa wanahakiki lakini kwenye meza ya NEC hapakuwa na udanganyifu wowote ndiyo maana hapakuwa na kasoro zozote zilizobainika.

Swali; Anayepiga kura ZEC, ndiyo yule anayepiga kura NEC. Kwa nini idadi iongezeke ZEC halafu NEC idadi ya wapiga kura isiongezeke.

Jibu ni kwamba, siyo lazima udanganyifu ufanyike kwa kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura, la hasha! Kuna uwezekano wa wapiga kura wakaingia na kura fake na wakafanikiwa kupiga kura zaidi ya moja kwa upande wa viongozi wa Zanzibar lakini wanapokwenda meza ya NEC wasifanye huo udanganyifu.

Pili Watumishi wa ZEC wanaweza kutoa balot paper zaidi ya moja kwa mpiga kura kwa lengo la kufanya udanganyifu kwa lengo la kupendelea wagombea wa chama fulani, na watumishi wa NEC wasifanye huo idanganyifu,

Tatu udanganyifu unaweza kufanyika wakati wa kuhesabu kura na kwa upande wa ZEC wakaongeza idadi ya kura lakini upande wa NEC wasifanye hivyo.

2 comments:

Anonymous said...

B/S Nenda rejea Matokeo yalotangazwa na NEC katika jimbo la Bumbuli tu ili ujifunze zaidi. Idadi ya walopiga kura imezidiwa mbali na kura walopata wagombea.
Acha kufanya watu wajinga. ZEC action siiungi mkono but atleast wameamua kusema black and white kuhusu issue nzima ya idadi ya kura na wapiga kura kuongezeka. Uchaguzi wote ni Batili si kwa wapiga kura, la hasha ni kwa walotaka kuendelea kutawala na kufanya ubadhirifu wa kuongeza kura na hapo ndipo wazungu wanakwambia numbers don't lie.
Maelezo ulotoa hayaondoi ukweli kuwa kuna kura za ziada zimeongezeka kwenye pande zote. So if there are sign of fraud in Znz automatically inaathiri uhalali wa kura za JMT. Ni ufahamu wa katiba na sheria ndo unaweza kukupatia mwanga kwenye hii issue.
Wamechemka kwa ufupi walotaka kuleta wizi wao cheap.

Anonymous said...

We mwenzetu shule gani umepitia unashindwa hata kujumlisha hesabu nyepesi kama hiyo? Au na wewe umeanza kuchanganyikiwa?

Kufuatana na rekodi za NEC, idadi ya kura zilizopigwa Bumbuli ni --------44,011

Wagombea walipata kila mmoja wao kama ifuatavyo:

ACT --------------- 447
ADC---------------- 188
CCM----------------35,310
Chadema------------ 7,928
CHAUMA------------- 85
NRA---------------- 15
TLP---------------- 13
UPDP--------------- 25
-------------------------
Jumla -------------44,011

Mwenzetu hebu tueleze wewe tofauti ya kura zote zilizopigwa huko Bumbuli na jumla ya kura wagombea walizopata inatoka wapi? Au wenzetu mnatumia makaratasi mengine ambayo NEC hawana? Na hii inaweza ikawa sababu mojawapo kwani nini mnalalamika!