Leo asubuhi Jaji Lubuva kabla hajaanza kusoma matokeo ngazi ya Urais ametolea ufafanuzi mambo kadhaa hasa suala la tume kutoa matokeo tofauti na matokeo yaliyopo majimboni. Lubuva kasema sio nia ya tume kwa wakati huu kuanza malumbano na vyama vya siasa au na wadau wengine lakini pale panapokuwa na upotoshaji mbaya, upotoshaji wa hali ya juu tume inalazimika kusema.
Jaji Libuva kasema matokeo yanayosomwa na tume ya uchaguzi yamechakachuliwa kuhusu wagombea wa Urais si kweli, kinachosomwa kimehakikiwa kwa yale ambayo yametokea katika majimbo, hayo ndio yaliyokuwa yamehakikiwa wakiwemo mawakala wa vyama mbalimbali, fomu imetiwa saini kwenye majimbo wakiwemo mawakala na kinachosomwa ni kilekile kilichopo katika majimbo yote.
3 comments:
Sio kweli kwani idadi inakinzana. Mungu aepushe yote.
I am pissed off, I am angry with my own COUNTRY, and the government of Tanzania, very undemocratic. African countries, especially Tanzania, Learn from hon Goodluck, transfer power peacefully, or else, you will be forced out...
You must have lost your mind, SOB! Who told you democracy means UKAWA must win? Do you want the government to transfer power to the losing candidate? You must be crazy! Your corrupt candidate is clearly nowhere close to winning the election even if 200K votes were arbitrarily alloted to him.
Post a Comment