Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25. Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi. Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku ya Jbila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
7 comments:
Asante mkuu. Tunatambua sote sisi ni wamoja na tuaeleweka kwa utulivu na amani tuliyojaliwa. Tukubali kuweka utulivu huo wa masaa 12 na kuendelea. Hatutapenda kuona nguvu za ziada zikitumika kama mabomu na risasi za moto kwa asiyekuwa na silaha. Kama akitokea nguvu ya kumkamata inawezekana tuhifadhi silaha kwa vita sio amani. Mungu atubariki.
Africa it's really Africa
They can't make they own decisions sorry
If you demean Africa so much why don't you migrate to another continent where you think it will best suit your ego?
Wheather in Africa or America people safety and security is the number one priority for every nation whenever a big event is concerned. Only an ignorant one can talk stupid about that.
Wewe ndugu @11:20AM, hatuelewi nini umeandika. Tafadhali rekebisha ulichokiandika ili ueleweke. Why use English when you don't have a good command of it? What are you trying to imply by the statement on Line #2 "They can't make they own decisions sorry" ?
unisaidie igp mwangu unasema nijifungie nyumbani ili wale unaowaona wanafaa kuranda-randa waingie na kutoka vituo vya kupiga kura.nakuuliza swali,mwisho wa siku kituo changu cha kupiga kura kina wapiga kura 450.kura zimehesabiwa ,zimepatikana kura 1200,yaani ziada ya kura [za wizi hizo ]750 hicho ni kituo kimoja tuu.jee wewe igp mwangu huoni ndiye utakaye kuwa umeuharibu uchaguzi mkuu wote wa tanzania wa mwaka 2015? Agizo lalo tunahisi,lina mkono mchafu sana,wa hila wa ccm.na hii imedhihirika kutokana na waraka wako kushabihiana sana na waraka wa januari makamba msemaji mkuu wa kamati ya kampeni wa ccm inayohusu taarifa ya ccm kufunga kampeni,isomeni wananchi,mtagundua jambo.
Chadema/Ukawa ngojeni miaka ijayo kama bado mtakuwa chama. Kwa sasa mmeonyesha bado hamjaiva hivyo Watanzania hawawezi kufanya kosa la kuwakabidhi madaraka.
Post a Comment