Advertisements

Thursday, October 1, 2015

Juma Nyosso alivyomfanyia kitu mbaya John Bocco



TOA MAONI YAKO JUU YA HII VIDEO MCHEZAJI HUYU KAFUNGIWA MIAKA MIWILI NA FINE MIL 2. JE UNADHANIA WOTE WALITAKIWA KUPEWA ADHABU?.
SOURCE:SHAFFIHDAUDA

5 comments:

Anonymous said...

Huu ni ujinga tena anatakiwa afungiwe kucheza soka miaka miwili na akirudia afungu\iwe maisha.Huyu sio mcheza wa soka bali ni muhuni na chama cha mpirakinafanya nini hadi sasa bila ya kumpa adhabu?Ignorant and also stupid.TFF let him go back to do other job he is not suitable for soccer in Tanzania.

Anonymous said...

2 years? it should be a life ban. It is a stupid thing to do in our culture. Shame on you Nyoso.

Anonymous said...

kufungiwa miaka miwili kwa kosa kama hili ni kifungo kikubwa sana kwa mchezaji. hiyo ni kulipiza kisasi na kumuua kimchezo huyo mchezaji. watanzania tukumbuke hii ni karne ya 21 sio yale mambo ya zamani mtu akikutwa na kipande kidogo cha bangi kifungo miaka 10. tuchukue mfano wa mchezaji mwengine duniani mwenye tabia za ajabu awapo uwanjani Luis Suarez amekuwa akingata wachezaji wenziwe mara nyingi tu lakini adhabu zake ni kufungiwa idadi fulani ya mechi za msimu, faini na pia kulazimishwa kupata matibabu ya kisaikologia na kiakili. miaka miwili ni mingi sana tena sana ni sawa ni kumuua kimchezo huyu mchezaji. makosa uwanjani yanatokea sana tu lakini tusitoe adhabu kama kulipa kisasi. tuwe na busara. ona hata miongoni mwa adhabu zake hakulazimishwa kupatiwa matibabu ya kisaikolojia na kiakili

Anonymous said...

HUyo Nyosoo ni wakufungiwa milele mpira kwake uwe historia na wengineo wenye tabia kama hizo waweze kuzisoma alama kwani kitendo alichofanya ni cha kishashi na hakikubaliki katika jamii.

Mwenzake amekuwa mpole tu je angeamua naye kupigana naye kiwanjani ingekuwaje? Si wangepasuana macho?

Anonymous said...

Sisi sio akina Suarez na jumuiya zao. Tamaduni zetu ni za muhimu sana na tunapenda kuzilinda. Wazo la huyo aliyeandika kuwa hii siyo karne ya 21 na hivyo mtu anaweza akamfanyia mwenzake kitendo cha utovu wa nidhamu namna hiyo ni wazo la mtu limbukeni. Tuache kukopi tabia za kigeni hasa pale tunapojuwa haziendani na maadili yetu. Pia ni upuuzi kuogopa kumuadhibu ipasavyo mtuhumiwa wa maadili potofu ati kwa ajili tu hivi leo tunaishi karne ya 21. Tabia bora, maadili mwafaka, heshima na upendo ni vitu muhimu sana katika jamii na ni vitu ambavyo havibadiliki kutoka karne moja hadi karne nyingine. Ukiona mtu anabadilika tabia zake kwa ajili ya madiliko ya karne ujue huyu ni ana tatizo na anafaa kuangaliwa.