ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 2, 2015

JUSSA MWANASIASA MWENYE KUONA MBALI

Na Swahilivilla. Blog Washington  Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema: "Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi...". Pia Waswahili wanasema: "Akili ni nywele"
Mshitakiwa Karama aliipinga hoja ya Waziri Majivuno kwa kusema: "....Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima..."
Nimekuwa nikiyatafakari mafungu hayo matatu ya maneno ili kuona kama yana uhalisia wowote katika maisha yetu ya leo.
Pichani Ndugu  Saidi Mwamende akimuliza swali   Mhe: Jussa,  (Hayupo Pichani)
Hivi majuzi swahibu yangu Said Mwamende alinipigia simu na mara tu baada ya kuijbu, nilihisi sauti yake imejaa furaha, ndipo nikamwuliza ''umepandishwa cheo?" Akanijibu: "Hapana, bali nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania zinavyokwenda na nikakumbuka ule mkutano wa Mheshimiwa Ismail Jussa alioufanya na Wanadiaspora hapa Washington. Yale aliyoyasema ndiyo yanayoendelea kutokea hivi sasa". Nikakurupuka kuchakura maktaba yangu kuitafuta rekodi ya mkutano ule ili nijikumbushe aliyoyasema Mheshimiwa Jussa. Baada ya kuiangalia tena, nikaona sehemu ambayo Swahibu yangu Said Mwamende alimwuliza Mheshimiwa Jussa swali ambalo lilihitaji mwono na mtazamo wa kina wa kisiasa: "Je, UKAWA, tuseme, kwa upande wa chama chako wewe atakuwepo Mheshimiwa Lipumba, na tuseme kwa upande wa CHADEMA Mzee wetu Mbowe. Watu hawa tayari wameshagombea Urais. Je hamuoni kwa CCM kwa sasa hivi kuna hombwe la aina fulani? Kuna Mheshimiwa Lowassa inawezekana kwamba hatogombea CCM kutokana na labda hawatomtaka. Mnafikiriaje UKAWA kama mtamchukua yule Lowassa ili mumuweke pale agombee?" Kwa ulimi wa fasaha kuliko wa Karama wa Kusadikika, Mheshimiwa Jussa alilijibu swali la Bwana Mwamende ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania katika Jiji la Washington na Vitongoji vyake (DMV), kwa kusema: "Katika siasa, wiki moja inaweza kuwa muda mrefu sana". Aliendelea kwa kusema kuwa siyo Lowassa tu, anaweza kupitishwa Loawassa akaachwa mtu mwengine mwenye ugomvi na Lowassa vilele. Kwa sababu CCM hivi sasa siyo chama tena kinachowaunganishwa na itikadi. Kinachowaunganisha ni Escrow na kwamba kila mmoja atapata mgao wake kiasi gani".
 Mhe: Ismail Jussa  akijibu swali la  Saidi Mwamende  (Hayupo pichani)
Katika mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu jijjini Washington, Bwana Ismail Jussa, aliwathibitishia Wanadiaspora wa Tanzania nchini Marekani pamoja na ulimwengu kwa ujumla kuwa Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima, lakini nadharia hiyo wakati wake umepita na hautorejea tena. Kwani katika kujibu swali la Katibu wa Jumuiya ya Watanzania kwaishio jijini Washington na vitongoji vyake Bwana Said Mwamende, Mheshimiwa Jussa alisema ni mapema mno kulitolea kauli swala hilo, ispokuwa "nitasema moja ambalo litatosheleza swali lako"
'Moja' hilo la Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mji Mkongwe, Zanzibar ambaye nywele zake bado ni nyeusi, linathibitisha kuwa nafasi hiyo aliyonayo kupitia ridhaa ya wananchi wa Jimbo lake hakuipata kwa sudfa tu, bali alistahiki na anaistahiki. Bali ni Mwanasiasa aliyekomaa na mwenye kuona mbali. "Nilisema mapema kwamba nazungumza na Mwenyekiti Mbowe, nazungumza na Mwenyekiti Lipumba na nazungumza na Mwenyekiti Mbatia. Sioni kwamba kwa wote hao kuna fikra ya ung'ang'anizi kwamba lazima niwe mimi". Alisema Bwana Jussa kwa kujiamni, na kusisitiza "Hilo silioni kwa sasa hivi". Upana wa wigo wa mawasiliano yake hayo unadhihirisha ukomavu wa akili yake, na kwamba fikra zake hazikufungika ndani ya vichochoro vya Mji Mkongwe, bali zimevuka Bahari ya Hindi na kuangaza Tanzania yote na hata nje ya mipaka yake. Mheshimiwa Jussa hakuwa anastawisha Baraza tu au 'kumwondosha njiani' Bwana Mwamende, bali alikuwa anazungumzia uhalisia wa mambo yanavyopaswa kuwa. Aidha hakuwa akitumia ulaghai wa kisiasa pale aliposema: "Na ninachojua ni kwamba viongozi wetu wanaangalia hata nje ya vyama katika kupata mgombea ambaye ataweza kuwakilisha vyema misimamo na ajenda ambayo UKAWA inaisimamia". Bwana Jussa ambaye kitaaluma ni msoni wa Sheria, alidhihirisha wazi kipaji chake cha kuweza kushtukia na kufichua mbinu sa kisiasa zilizojificha. Aidha si mtu anayekhofu kuelezea maoni yake binafsi kwa manufaa ya umma. Haya yanaonekana alipoendelea kunena: "Nikwambie kitu kimoja, hili ni mawazo yangu binafsi: 'Mimi nahisi CCM wana khofu na hilo unalolisema kama Chama. Na ndiyo maana tulikuwa tunajua sote kwamba CCM ilikwisha tangaza kwamba Mkutano wao Mkuu wa kumpata mgombea ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi wa April. Lakini juzi tulimsikia Nape Nnauye akisema kuwa kutokana na sababu ya kura ya maoni, na Bunge la Bajeti linofuata baadaye, itakuwa vinaingiliana. Kwa hivyo bora uakhirishwe mpaka baada ya Bunge la Bajeti'.." Kigogo huyo wa Chama Cha Wananchi CUF, aliitafsiri kauli hiyo ya CCM kama ni mbinu ya kuvuta wakati na kwenda karibu na uchaguzi wakidhani wataweza kuliepuka jambo hilo. "Kwa hiyo, tafsiri yangu ni kwamba wanataka kwenda zaidi, ili wakidhani wataweza kuliepusha hilo" Alichambua bwana Jussa ambaye kadiri nywele zake zinavyopotea, ndivyo akili zake zinavyozidi kukomaa.
Pichani Makamu Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Mwakilishi wa sasa wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa.
Tangu ujanani mwake, Mheshimiwa Ismail Jussa alikuwa akipenda kukaa na watu wazima akijua kuwa huko ndiko kwenye hazina za hekima na maarifa. Mwenendo wake huo, ndio uliopanua muono wake na kuweza kuichambua CCM na kuielezea kuwa ni Chama kilichopoteza mwelekeo, itikadi na misingi kiliyoasisiwa chini yake, na kwamba kilichobaki ni makundi makundi ndani yake yenye kupigania maslahi binafsi.
"Kwa jinsi ninavyoona, ile CCM ya Nyerere ambayo mpo pale kwa sababu ya Ujamaa na Azimio la Arusha haipo tena. Kilichobakia ni kwamba ni vipi kila mtu na kundi lake na rafiki zake watafanikiwa kupata nafasi wakavuruge nchi"
Jussa si mtu wa papara wala pupa, bali mtu ni mwenye subira, na alimtaka Bwana Mwamende kujiunga naye katika mbuga ya subira na kuupa nafasi wakati ufanye kazi yake.
"Kwa hiyo ninachosema, hayo tuyaachie wakati wake ukifika. Kama atatoka miongoni mwa hao, kama atatoka nje ya hao, au kama atatoka miongoni mwa viongozi wa UKAWA tuuachie wakati utasema".
Aidha kwa mara nyengine alisisitza imani yake juu ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA juu ya msimamo wao wa kuwa na mgombea mmoja:
Nataka nikuhakikishie kuwa kwa upande wa UKAWA si hoja kwamba awe Lipumba, Slaa, Mbowe au Mbatia. Si hoja kabisa kwa sasa hivi. Hoja ni nani ataweza kubeba bendera ya UKAWA"
Mheshimiwa Jussa alimalizia jibu lake kwa kusema "Nadhani tutafika vizuri".
Kauli hiyo ilikuwa inatabiria "Safari ya Matumaini" ya Mheshimiwa Edward Lowassa iliyogeuka na kuwa "Safari ya Uhakika".
Naam, akili si nywele, na wala mvi si dalili ya hekima. Bali elimu ndiyo mwangaza, khaswa pale inapotiliwa nguvu na tabia ya kukaa na watu wenye busara. Maneno aliyoyasema Mheshimiwa Jussa tarehe 28 Februari 2015 nchini Marekani, ndiyo ambayo leo hii yanatuongozea siasa za Tanzania.

7 comments:

Anonymous said...

Muandishi wa makala hii umechanganya vitu mno hauleweki, aujui jinsi ya kupangilia maelezo yako , nafikiri inabidi ujifunze kuandika kwa kufata mpangilio wa 1,2,3,4, na mwisho kumalizia maelezo yako ,makala yako inaweza kua na maana lakini ulivyo changanya msomaji akianza kusoma tuu kidogo ataki kuendelea ,kutokana na mfumo wa maelezo ulioyandika , jamani kama mnataka kuwa waandishi wa habari nendeni shule .

Unknown said...

Uana siasa gani wa kuona mbali aliokuwa nao Jussa zaidi ya kuwa master mind na kamanda wa mwamsho? Si shangai kabisa kuona lowasa anawatetea wale viongozi wa mwamsho hadi anathubutu kusema yupo tayari kuvunja amri ya mahakama kwa kuwaachia huru hao magaidi wa kundi la mwamsho iwapo akichaguliwa kuwa raisi. Hayo ni mapendekezo ya Jussa kwa kumtumia lowasa wanaimani malengo yao ya kuendeleza siasa zao za chuki na zilizopitwa na wakati Zanzibar yatatamia. Jussa smart kwa lowasa lakini si kwa wanzanzibar wanamfahamu kuliko anavyojifamu yeye mwenyewe. Jussa na vibaraka vyake walishampima lowasa na kujuwa ni miongoni mwa watu dhaifu sana ni mtu ambae wanauwezo wa kumpelekesha wanavyotaka lakini sio magufuli na CCM. Magufuli smart huwezi kuja kumshauri sijui tuwaachie wahalifu kwa utashi wa kisiasa alafu uwe rafiki yake hicho kitu hakiwezi kutokea kwa magufuli.
Huyo Jussa fikra zake zimegubikwa na msongo wa mawazo wa kihizbu na siasa za kimatabaka. Kama ni mvi ni dalili ya akili na busara basi vile vile ni moja ya ishara nzuri ya ufisadi.

Anonymous said...

Ndugu yangu maoni yako tungeyapa uzito mkubwa kama Kiswahili chako kingekuwa fasha. Lakini unamkosoa mwandishi, wakati misitari michache uliyoandika yamejaa makosa ya kitahajia. Ingelikuwa vizuri kwanza kuiangalia lugha yako, halafu watu watakuja kusoma kwako uandishi.
Nimalizie kwa kusema "jua litaendela kung'ara ikiwa mlemavu wa macho ataiuona mwanga wake au la"
Nakutakia siku njema.

Anonymous said...

@ Sallen Marlon

Hivi wewe mwehu? Sasa unasema Lowasa anaweza kupelekeshwa. Hivi humuoni huyo mwehu mwezio Magufuli anavyopelekeshwa na Mulembo ati anaambiwa apige push up mara anaruka jumping jacks.Na kuhusu Jussa ni mtu makini ndio maana inakuuma,Halafu unaongelea kuwa Uamsho ni magaidi kwa lipi walilolifanya hata ukawaita magaidi kwa ushahidi upi ulio nao? manake hata Mahakama mpaka leo hawajawahukumu. Kama una ushahidi wowote weka hapa au kama unayo japo video walioongelea kuhusu ugaidi weka hapa tuione basi.

Anonymous said...

Mwandishi wa October 3, 2015 at 3:31 PM - Hawa walioko jela mpaka leo kama siyo magaidi ni nani? Hivi siku hizi jela nazo zimegeuka kuwa guest house kuwa mtu unakwenda kupanga kwa ridhaa yako?

Mwandishi wa October 3, 2015 at 1:11 AM uliyoandika ni sahihi kabisa.

Anonymous said...

We mpumbavu kwa kuwatetea hao mwamsho unakiri kwamba jusaa ni kamanda wa mwamsho?
Kuhusu kundi la mwamsho kuwa kikundi cha magaidi au la?
Wewe sijui ni mtanzania kutoka sehemu gani? Nna wasi wasi pengine unatokea ruwanda sio Tanzania hata ushindwe kufahamu kuwa mwamsho si kikundi cha ugaidi kilicho husika na kuwamwagia watu acid , kuendesha mashambulizi zidi ya viongozi wa dini, kuendesha campaign ya mambano zidi ya vyombo vya usalama na mambo mengi machafu yaliokuwa hayafai kwa jamii iliostaraabika kama ya wanzanzibar.
Hata hao mwamsho wenyewe wanajua kwamba zambi ndizo zilizowapeleka gerezani. Huwezi kujifanya kiongozi wa Dini alafu kumbe unaajenda zako nyingine halafu mwenyezi mungu akutazame tu asikuadhibu. Hakuna jambo baya na la kipumavu kama kujaribu kumcheat mwenyezi mungu. Kuhusu magufuli kupiga push up, magufuli mtu wa watu bwana he! atakavyofanya watu wana mkubali. Kwani wewe kwa ujinga wako unafikri Lowasa hazitamani push up? Lowasa angependa sana kushoo off na push up how fit he is, ila ubavu hana, yule mzee hata kujisaidia kwa taabu ataziweza kweli push up lol. Bila ya kutumia utashi au ukosefu wa kutotambua usiku na mchana tofauti zake kati ya magufuli na lowasa kwa kila Kitu basi magufuli ni bora zaidi ya lowasa, kwa elimu, uadilifu, uchapa kazi, afya, communication skills, subira, working accomplishment na mengi tu sasa watu wa lowasa na ukawa naamini mnaelewa hivyo kuwa magufuli ni bora mara nyingi kuliko lowasa isipokuwa nyinyi ni watu mliokuwa very cheap mnakubali kudanganywa danganywa kama watu mlioazimwa akili kuzitumia mnaogopa mnangoja mweye akili zake aje kukuelekezeni jinsi ya kuzitumia, sasa kwa hali.hiyo mtasubiri sana.

Anonymous said...

Haisaidii kuendelea na matusi yenu dhidi ya Magufuli kwani mpende, msipende hivi karibuni tu atatinga Ikulu na atakuwa kiongozi wetu wote - tunao muunga na msio mmuunga mkono. CCM Oyeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!