Monday, October 26, 2015

Kasoro zachelewesha utangazaji matokeo Iringa Mjini

By BerdinaMajinge
Iringa. Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Ahmed Sawa ameahirisha kutangaza matokeo ya ubunge katika jimbo la Iringa mjini na kuahidi kuyatangaza kesho baada ya kurudiwa kwa uchaguzi katika kituo cha ipogolo c namba mbili manispaa ya Iringa.

Akitangaza uamuzi wa kurudiwa kwa upigaji kura katika kituo hicho msimamizi huyo amesema hatua hiyo inaafuatia kutokea dosari iliyosababishwa na kuporwa kwa masaduku ya kura ya mbunge na rais katika kituo hicho jana wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea.

Mapema leo asubuhi wananchi walifika kusubiri kutangazwa kwa matokeo hayo ambao baada ya kusubiri kwa muda mrefu walianza kuimba nyimbo mbalimbali kushinikiza kutangaziwa matokeo hayo.

baadaye mkurugenzi wa manispaa ya iringa ambaye ni msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la iringa mjini alitoka kuwaeleza wananchi sababu ya kutotangazwa kwa matokeo hayo huku akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi.

“Hatutaweza kuwatangazia matokeo ya ubunge leo kutokana na sababu zilizo nje wa uwezo wetu na tunafuata sheria na taratibu za tume ,licha ya Mchungaji Msigwa kuongoza katika kura lakini hatutaweza kumtangaza mshindi mpaka kituo hicho kirudiwe”alisema

Baada ya kushindwa kusikilizana msimamizi huyo aliomba mbunge anae naliza muda wake kuzungumza na wananchi hao na kuwaoomba watawanyike hadi hiyo kesho baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio.

Kwa upande wake mchungaji Peter Msigwa ambaye ndio mshindi katika jimbo hilo akiongoza kwa zaidi ya kula 6,000 dhidi ya wapinzani wake alisema kuwa kutokana na tatizo hilo mkurugenzi hana mamlaka ya kutangaza mshindi mpaka atakapo kituo hicho kitakapo rudiwa.

“Makamanda wangu kuweni wapole na wasikivu mkurugenzi hawezi kutangaza matokeo yakiwa nusu hvyo kesho asubuhi mkapige kura ili tupate matokeo ya ushindi wetu kiharali”alisema

“Naomba kesho mje saa kumi jioni kupata matokeo,kwa sababu tumeshinda hata msipoenda kupiga kura bado ushindi tunao,hivyo nawaomba mtawanyike kwa amani na kesho tutaomba kibali polisi kwa ajili ya kushangilia ushindi na hatutapigwa mabomu”alisema

Kituo hicho cha ipogilo C kinajumla ya wapigakura 258,ambapo chadema walikubali kuwaachia upinzani kura hizo 258 ambazo zilileta matatizo ili wakubali kusaini na kutangaza matokeo lakini walikataa na kudai uchaguzi urudiwe jimbo zima la Iringa.

Wananchi hao ambao walifika katika ofisi ya manispaa ya Iringa kwa ajili ya kusubiri matokeo ya mbunge wao walikaa kwa utulivu zaidi ya masaa 11 huku wakiimba nyimbo tofauti bila kuleta fujo katika eneo hilo.

Hata baada ya kutangaziwa kuwa matokeo hayo hayatatangazwa leo kutokana na kura kupotea katika kituo hicho walikubali na kuwa watulivu na hatimae kusambaa katika eneo hilo kwenda kuendelea na majukumu yao na kuahidi kurudi kesho kama walivyoambiwa na mkurugenzi.

MWANANCHI


No comments: