ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 11, 2015

Kongamano la kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo lafanyika Pemba

MRATIBU wa kongamano la kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, Khalfan Amour Mohamed lililofayika mjini Chake chake, na kutayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Afisa mipango wa ZLSC Siti Salim Habibu na kushoto ni Afisa Mdhamini wizara ya Katiba na Sheria Omar Khamis Juma akifuatiwa na Mratibu wa ZLSC, Fatma Khamis Hemed, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASHIRIKI wa Kongamano la kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo, ambalo hufanyika kila ifikapo Oktoba 10 ya kila mwaka, ambalo limefanyika mjini Chake chake na kutayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba.
MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akielezea jambo kwenye kongamano la siku moja la kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo, kulia ni Mratibu wa Kongamano hilo Khalifan Amour Mohamed na katikati ni Afisa Mdhamini wizara ya Katiba na sheria Pemba, Omar Khamis Juma.
AFISA Mdhamini wizara ya Katiba na Sheria Pemba, Omar Khamis Juma akifungua Kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, lililotayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Afisa Mipango wa ZLSC Siti Salim Habibu na kushoto ni Afisa Mipango wa ZLSC Fatma Khamis Hemed.
MSHIRIKI wa kongamano la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, Ali Amour Makame kutoka afisi ya DPP, akichangia jambo kwenye kongamano hilo lililotayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na kufanyika mjini Chake chake.
MSHIRIKI wa kongamano la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, ambae ni mwafunzi wa Chuo cha ZCBE akichangia jambo kwenye kongamano hilo lililotayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na kufanyika mjini Chake chake.

No comments: