Monday, October 26, 2015

LOAWASSA ALONGA NA WANAHABARI

Nimewaita kueleza masikitiko yetu mawili
Haswa katika upande wa jeshi la polisi

Tuna vijana wetu wanaofanya kazi za IT kwa kujitolea maeneo ya kinondoni na kijitonyama jumla ya vituo vitatu

Hawa vijana wanafanya uzalendo,kushiriki katika uchaguzi wa nchi yao,na kujenga historia moya ya nchi yao,tendo la kuwakamata si la haki kabisa

Wamewavamia na kuwakamata kwa kosa la human trafficing ambalo ni kosa kubwa na halifanani na kazi wanazofanya

Nimeona taarifa zao za matokeo ya kura wameanza kuonyesha watu taratibu zinazompendelea magufuli 

Ningependa kuwashauri tume watoe matokeo yote kwa pamoja
Sio kufanya kama hivi wanavyotoa kidogo kidogo yanayoongelea upande wa pili kushinda,wanafanya maandalizi ya kisaikolojia ( psychological preparedness) kudhoofisha morali ya wafuasi wa UKAWA ambayo si haki

Swali
Give us your view So far on the tallying

Jibu
so far so good 50/50
Ila napenda kutoa pongezi kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi kupia kura,
Wamekua watulivu na kuheshimu sheria na kanuni.

Swali
You said the main tallying station has been raded
Do you have an alternative ?

Jibu
We have no alternative ,We have been handcaped
They have been so unfair
I wish i could charge them in ICC

Swali
Chadema ina mpango gani kuwatoa hao waliokamatwa?

Jibu
Jumla yao walikua 191 wanajumlisha kura.
Sisi hatuna hatua stahiki zaidi ya kuongea na nyie waandishi wa habari mpeleke taarifa hizi duniani.
Kwamba huu ni uonevu mkubwa

9 comments:

Unknown said...

Walichofanya police sawa sawa kabisa kwa sababu ni watu hawa hawa au wanawaita vijana wa IT ndio waliokuwa walitengeneza matukio feki ya kukamatwa kura feki sasa leo utawaamini vipi kutoa matekeo halali ya kura ? Lengo ni kutengeneza matokeo feki kitaifa hata kama ukawa wameshindwa na kupekea maandamano na vurugu nchini. Tanzania ni nchi ya sheria sio nchi ya kihuni kila mtu ajifanyie anavyotaka.

Anonymous said...

Kuanzia neno Swali je unauhakika aliyaongea hayo au umeyakupua ulikokwapua na kuyabandika hapa!!! Tafuta ukweli kabla kubandika.

Anonymous said...

Simwelewi ndugu Lowasa, kwa nini asisubiri matokeo ya tume kama sisi Watanzania wenzake? Hao so called Vijana wa IT are paid followers recruited primarily to spread propaganda and chaos.They were under the radar of Tánzania intelligence svc long before yesterday's arrest. kudos to TZ police for keeping us safe!

Anonymous said...

Kwakuwa Lowasa alitamka kuuchukia umaskini na kuonyesha nia ya kuwakomboa mama ntilie na bodax2, natumai at a endeleza harakati hizo nje ya uraisi .ie kufungua entity itakayo wakomboa.au!

Anonymous said...

Kuna tofauti kubwa kati ya tallying centre na ciber manipulation centre.

Anonymous said...

Na utawaamini vipi tume ya NEC ya ccm? Na kwa nini hao polisi wa ccm hawakuvamia kituo chao cha ccm hapo mlimani city. Nyie ccm acheni zenu hizo. Nyie ndio mnao sababisha vurugu then mnawalaumu watu wengine.

Anonymous said...

Mdau kama huujui uliza kabla ya kuanza kulalamika, hiyo ya Chadema haikuwa poll tallying ccentre or anything. Ulikuwa ni uhuni,ulio na lengo la kutawanya propaganda na hatimae kuvuruga uchaguzi.

Anonymous said...

Nyie mlie tu kwani malalamiko na manung'uniko yenu sasa tumeshayazoea ila ukweli tu ni kuwa hayatawasaidia. Mmesha peleka malalamiko Umoja wa Mataifa na kwingine subirini muone kama watasaidia. Ujue tu kama hujaona au kusoma kokote, wasimamizi wa jumuiya za kimataifa waliokwenda nchini na waliohojiwa na vyombo vya habari mbali mbali tayari wameshatoa tathimini yao ya awali wakisifia NEC, serikali na Watanzania kwa ujumla kwa kuendesha uchaguzi ulio shwari na tulivu. #Hapa kazi tu.

Anonymous said...

Bankruptcy ya Mhe. Lowassa. Hebu akasome kazi za ICC ni nini? "I wish i could charge them in the ICC"!!! What a shame. Hivi mswahili yeyote mambo yakimuwea magumu sharti amkimbilie mzungu? Watanzania kumbe hawakukosea kumchagua Magufuli. Thank God.