Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mbeya katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Oktoba 18, 2015.
4 comments:
Mbona sioni wanamuziki wa bongo flava kwenye hizo picha?
LEO NI SIKU YA JUMATATU TAREHE 19 OCTOBA 2O15,TUMEBAKIZA SIKU SITA TUU YAANI CHINI YA WIKI ILI TUIFIKIE SIKU YETU YA KUPIGA KURA WATANZANIA YAANI JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015.MABIBI NA MABWANA SALAAM ALEYKUM,TUMSIFU YESU KRISTU .JINA LANGU NAITWA KIUNGWA MILEMETWA.NIMEVUTIKWA LEO NISEME MANENO MAZITO SANA WAKATI HUU TUNAPOJIANDAA KUMCHAGUA RAIS WETU,MBUNGE WETU NA DIWANI WETU.HAWA MBUNGE NA DIWANI NI VIONGOZI WA MSAADA KWA MWENYE SERIKALI YAANI MSHIKA DOLA MHESHIMIWA RAIS.KWA MUJIBU WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA SASA,MHESHIMIWA RAIS ANAPEWA UWEZO NA MAMLAKA MAKUBWA SANA KATIKA KUIONGOZA NCHI NA WANANCHI.RAIS AWE AMEJAALIWA KARAMA,MTULIVU,MKIMYA ANAYETAFAKURI NA KUZIJIBU CHANGAMOTO MBALI MBALI KWA BUSARA YA HALI YA JUU,AEPUKE JAZBA NA UROPOKAJI,ASIJIWEKE KITUKO,AWE NA MWANDANI MSAIDIZI WA MFANO KATIKA HURUMA NA UONGOZI MBADALA AMBAYE NA SISI TUMEKWISHA MUONA,RAIS WETU AWE JASIRI ANAYEIELEWA PESA VIZURI NA MBINIFU WA VYANZO VYA MAPATO ILI KUUJENGA UCHUMI WA WANANCHI NA NCHI.MIMI MILEMETWA NIMEKWISHA MUONA SI MWINGINE BALI NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA NA MAMA YETU ALIYETOKEA GHAFLA TUU KUWA KIPENZI WA WATU KWA UCHANGAMFU,BASHASHA NA HEKIMA ZAKE KUBWA KATIKA KUZUNGUMZA NA KUCHAPA KAZI, MAMA REGINA NGOYAI LOWASSA.NIMEWAONA.EWE MWENYEZI MUNGU UTUJAALIE TUIONE NA TUIVUKE SIKU HIYO SALAMA SALMINI EEMIN.
Watu wengi sanaa
Watu wengi mmewaona lakini hao mliowaona hawatawasaidia kuingia Ikulu kwani wananchi tayari wameshaamua kumpa kura Magufuli.
Post a Comment