Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.
Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt
Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na
kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu
akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani
Karume.Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini
Unguja.
PICHA NA MICHUZI JR-PEMBA
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao.
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt
Mohamed Shein akiwahutubia
wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja
wa Gombani ya Kale mjini Pemba.Dkt Shein amewataka wakazi wa Kisiwani Pemba
kuilinda amani iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuwa Wananchi wakajitokeze kwa
wingi kupiga kura siku ya Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu Mwaka huu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana Mama Shadia Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo kisiwani Pemba.
Umati wa wakazi wa kisiwani Pemba kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kiswani Pemba wakifuatilia mkutano wa kampeni
uliofanyika jioni ya leo,kwenye uwanja wa Gombani ya kale kisiwani humo.
Wananchi
wa kiswani Pemba wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli pamoja na
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
walitumia jukwaa na mkutano huo kuwaomba kura za kutosha ili wakaiongoze
Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
1 comment:
Ahsante sana raisi mtarajiwa magufuli. Pemba na unguja wewe hasa ndie mwenye kura zao hao wengine walikwenda kuzurura tu.
Post a Comment