ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 11, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KIKAO CHA DHARULA CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR

Vigogo wa Chama Cha Mapinduzi CCM, waliokutana kwa dharura kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, walivalia kofia maarufu zijulikanazo kama "Mpama", ambayo hupendelewa kuvaliwa na Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli. Style hiyo ya uvaaji wa kofia ilionekana wakati wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya chama hicho kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya CCM Lumumba. Pichani Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, (katikati), na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinan Oktoba 10, 2015.
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (kulia) akiagana na Katibu Mkuu wa CCM, Abrahman Kinana, nje ya Ukumbi wa CCM Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Kikao cha dharula jana Okt. 10, 2015. Katikati ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Salim Ahmed Salim
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya wajumbe wa CCM kusimama na kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki, marehemu Celina Kombani, wakati wajumbe hao walipokutana kwa dharula jijini Dar es Salaam, Okt 10, 2015.
 Picha na OMR

1 comment:

Anonymous said...

Watakutana sana Kila saa Kila siku
Lowassa ndo agenda
Ngombale kawatenda
Na bado
Wiki tatu hizi atayasema mengine