Advertisements

Saturday, October 3, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA SHULE YA SEKONDARI J.K.NYERERE HUKO TARIME

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Capt. Mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo tarehe 2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi Shule ya Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa North Mara Gold Mine tarehe 2.10.2015.
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari J K Nyerere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Mara na wanachi wa Kijiji cha Myamwaga kusherehekea uzinduzi rasmi wa Shule ya J.K. Nyerere iliyojengwa na North Mara Gold Mine.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha Nyamwaga.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete baada ya kukata utepe hapa anakiondoa kitambaa kukamilisha sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Ndugu Jimmy Ijumba, Meneja wa ACACIA –North Mara Gold Mine mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo tarehe 2.10.2015.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga ikiwa ni ishara ya kuagana nao baada ya kuifungua rasmi Shule ya Sekondari J.K. Nyerere iliyoko katka Wilaya ya Tarime.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati akiingia eneo la Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwenye uzinduzi wa uboreshaji wa miundombinu katika hospitali hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Capt. Mstaafu Aseri Msangi na Ndugu Glorius Luoga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuondoa kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa uboreshaji wa hospitali hiyo.
Baada ya kuzindua rasmi uboreshaji wa hospitali ya Wilaya ya Tarime, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete anapanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo la hospitali hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na wanachuo wanaosomea uuguzi katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
Akina mama waliojitokeza kuja kuongea na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakicheza kwa furaha mara baada ya Mama Salma kuingia ukumbuni.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,Mama Salma Kikwete akiwapungia kwa furaha akinamama wa Tarime muda mfupi kabla ya kuongea nao tarehe 2.10.2015.

No comments: