Advertisements

Friday, October 9, 2015

MAMA SALMA KIKWETE KWENYE MIKUTANO YA KAMPENI MCHINGA NA LINDI MJINI.

1
Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi kwa ziara ya kikazi mkoani humo tarehe 8.10.2015.
2
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Mchinga waliokusanyika kwenye Kijiji cha Kikomolela Kata ya Matimba kwa ajili ya mkutano wa kampeni kwenye Jimbo hilo tarehe 8.10.2015.

3
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye kijiji cha Kikomolela kilichoko katika Jimbo la Mchinga, Wilayani Lindi kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 25.10.2015.
5
Mamia ya wananchi wa Kata ya Matimba iliyoko katika Jimbo la Mchinga waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mama Salma Kikwete.
6
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya kabila la Wamwela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mchinga tarehe 8.10.2015.
7
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi Ndugu Ali Mtopa akiongea na wananchi wa Kata ya Matimba waliokutana katika Kijiji cha Kikomolela kilichoko katika Jimbo mla Mchinga kabla ya kumkariribisha Mama Salma Kikwete kuhutubia mkutano wa kampeni tarehe 8.10.2015.
11
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia kwenye mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la Mchinga huko Lindi Vijijini tarehe 8.10.2015.
13
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dr. John pombe Magufuli kwa wananchi wa Lindi Mjini kwenye nmkutano wa Kampeni uliofanyia kwenye Kata ya Rasibura tarehe 6.10.2015.
10
Mjumbe wa NEC na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu Said Mtanda kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji cha Kikomolela tarehe 8.10.2015
8
 Mamia ya wananchi wa Kata ya Matimba iliyoko katika Jimbo la Mchinga waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mama Salma Kikwete.

PICHA NA JOHN LUKUWI

4 comments:

Anonymous said...

kwenye picha hii nawaona watoto wa shule wengi sana yaani ccm mmekosa watu wazima na kudhurumu muda wa masomo wa watoto wetu,kisa ati waonekane watu nyomo-nyomi-ccm,aibu tupu

Anonymous said...

Subiri tarehe 25/10 ndio utajua, kama wapigakura ni watoto au watu wazima..

Anonymous said...

ya nini kusubiri,tuzungumzie picha hii,nimesema mmekusanya watoro wa shule,nyinyi ni makatili mnawaharibia pia walimu ratiba nzima ya vipidi-elimu.ijibu picha,mbona unakwepa mada,utaendelea kuwadanganya watanzania wasioelewa kama wewe.tuna wiki mbili tuu ufunge mdomo kwa miaka mitano.

Anonymous said...

Ni kweli tarehe 25/10/2015 utaufunga mdomo pale CCM itakapo rejeshwa madarakani tena..