Nyumba ya familia, inayokaliwa na bibi
Siajabu Adam Ali wa kijiji cha Minazini shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake
chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake, Zahara Hamza Adam
kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba hiyo iliteketea kila kitu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Sehemu ya ndani ya nyumba ya familia,
inayokaliwa na bibi Siajabu Adam Ali na watoto wake wawili, kijiji cha Minazini
shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake Zahara Hamza Adam, kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba
hiyo iliteketea kila kitu.
Baadhi ya vitu vilivokuwemo ndani ya nyumba
anayoishi Siajabu Adam Ali, ikiwa ni pamoja na magodoro, mabegi mawili ya nguo,
vitanda, baiskeli na vyombo vya matumizi ya ndani, vikiwa vimeteketea, baada ya
nyumba hiyo kudaiwa kuchomwa na mmoja wa familia wa nyumba hiyo, Zahara
Hamza Adam kwa ugomvi wa kiamilia na sasa anashilikiwa Polisi.
Siajabu Adam Ali akizungumza na waandishi wa
habari juu ya mkasa wa nyumba ya familia anayoishi, baada ya kuchomwa na
mdogo wake Zahara Hamaza Adam, usiku wa kuamkia juzi, kutokana na hitilafu zao
za kifamilia, na kuiteketeza yote na hakukuwa na mtu aliejieruhiwa.
No comments:
Post a Comment