Thursday, October 22, 2015

NAPE APATA AJALI




KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.

Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.

Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.




Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."

Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.

GPL

4 comments:

Anonymous said...

Yaliagizwa magari 50 ya aina hii,TOYOTA maalum kwa ajili ya campaign high resolute team ya ccm.thamani ya gari moja kama hili alilopata nalo ajali nape ni million 360 kwa gari moja.kwa hiyo ccm wametumia billion 18 kununua magari ya kampeni tuu.sheria ya msajili wa vyama vya siasa nchini tanzania kuhusu ceiling ya matumizi[yaani kikomo cha juu] ya kampeni kwa mgombea urais ni billion 17.hivyo kwa magari haya ya kifahari pekee,narudia magari peke yake ccm yamevuka uhalali wa matumizi ya mgombea wao kwa billion moja.kwanza vuta pumzi.haya tuendelee,helicopters sita[6],mabango alfu hamsini.fulana,kofia na bendera million tatu,wanamuziki na wasanii zaidi ya 820 billion sita hadi nane,majukwaa na vyombo nchi nzima billion nne,kukodi mahoteli nchi nzima billion nane[8 billion],kuwalipia ghrama za kampeni wagombea wake nchi nzima billion nane,kuwanunua wapinzani legelege[kama dr.slaa,lipumba- siri ya bei wanaijua wao.FANYA MAJUMUISHO UKIFIKA TRILLION MBILI,SIMAMA USIENDELEE KWA SABABU UTAZIDI KUPANDWA NA GHADHABU.CCM NI WEZI WAKUBWA,WAKUBWA SANA,WAHUJUMU UCHUMI WAKUBWA.WAMEITUMIA HAZINA YA WATANZANIA WOTE,NA BENKI KUU KAMA MALI BINAFSI YA CCM.WANANCHI TUPO PAMOJA NA MUNGU WETU.SIKU YA UKWELI HAIKO MBALI.

Anonymous said...

Hivi nape anafanya kazi wapi kuweza kununua gari lenye dhamani ya million 200 sidhani kama kazi yake ya CCM ni ya kulipwa. Hii dalili tocha mfumo wa CCM kuondoka mwaka huu. Huu ni mfano mmoja na mdogo sana kuna zaidi ya maelfu ndani ya CCM.

Anonymous said...

Jamani gari LA milioni 360 likwapi hapo tena Toyota mi naogopa msidanganyike fanyeni utafiti kabla ya kuandika hizi habari

Anonymous said...

USIONE AIBU KUTAJA BEI YAKE,MIMI NIMEITOA TAKWIMU HII TOKA TOYOTA JAPAN 1 UNIT USD 165,000 KABLA HALIJAPAKIWA KWENYE MELI.HEBU NA WEWE,USIOGOPE,TUPE BEI.UNAELEWA WEWE BEI YA MAGARI HAYA KULIKO MIMI.HEBU ONDOA PUSH-UP ZAKO.