Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya
makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume,
ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa
Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akizungumza na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania
wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia
moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo
Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili
ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na
nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa
ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo
wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa
sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya
Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya
vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla
ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa
mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia
kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14
Novemba, 2015
No comments:
Post a Comment