ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 20, 2015

RAIS KIKWETE ALIKABIDHI JESHI LA POLISI MAGARI MAPYA 399 KATI YA 777 YALIYOAGIZWA

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe, IGP Ernest Mangu wakati akikagua sehemu ya magari mapya 399 kati ya 777 aliyokabidhi kwa jeshi la polisi leo Jumanne Oktoba 20, 2015 huko katika Chuo cha Polisi Kurasini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

12 comments:

Anonymous said...

Maandalizi yya Uchaguzi wa kutokukubali au vita ya wenyewe kwa wenyewe. Dola na wananchi walipa kodi??!!

Anonymous said...

walengwa wa magari haya ya kushambulia,kujeruhi na..... ni sisi raia tunaotembea mfukoni tukiwa na vitambaa vyeupe.ikumbukwe hapa duniani hakuna vitisho na udikteta vilivyowahi kudumu hata kwa muwongo mmoja.leo hii jumanne tarehe 20 octoba 2015 tukiwa tumebakiza siku tano tuu tuufikie uchaguzi mkuu magari-silaha yanakabidhiwa kwa polisi.magari haya hayapelekwi mipakani,hapana.wanasema ni ya kupambana na wananchi kwa tafsiri ya kufanya fujo.yote kwa yote,tuangalie mbele.tuna siku nne sasa,raia tukiwa tumebeba vitambaa vyeupe ishara ya amani,hapo jumapili tutajitokeza kwa wingi wa mamilioni kutimiza haki yetu kuu ya kikatiba, kupiga kura,kumchagua rais MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA,pia kuwachagua wabunge na madiwani, TUTAKWENDA VITUONI KWA AMANI KUBWA MNO,NA KWA UTULIVU MKUBWA MNO TUKIJUA AMANI NDICHO CHANZO CHA USHINDI WETU.

Anonymous said...

Kweli mheshimiwa Raisi umetufikisha hapa tulipo!! Kinamama tutaendeleakujifungulia chini na kufa kwa sana hata ambulance hakuna. Mungu aendelee kubariki ninyi!!

Anonymous said...

Migari yote ya nini wakati TANZANIA ni nchi ya amani?kwa nini hizo hela msijengee zahati katika kila kijiji?

Anonymous said...

Bila amani hata hospitali si salama.Gongera serikali kwa kuwapa polisi vitendea kazi.

Anonymous said...

Amani ni dynamic. Hata polisi wa Uswiss wako well equipped.

Anonymous said...

Sasa shida ni nini? kama wewe si mvunjifu wa amani you don't have to worry about magari. .

Anonymous said...

Hueleweki,ondoa hangover kwanza then rudi usome ulichoandika.

Anonymous said...

Shukurani za punda ni mateke. Kuna binadamu wengine hawafurahishwi na chochote kile kazi yao kulalamika tu hata wakitendewa mazuri ya aina gani. CCM na serikali yako endelea kufanya mazuri na kutuletea maendeleo nchini kwetu na tunakushuuru sana kwa hili.

Anonymous said...

Kwanini mambo hayo yoote wangoje uchaguzi. Walikuwa wapi siku zote.

Anonymous said...

Shida yako ni nini.kwani polisi kuwa na magari kabla,wakati na baada ya uchaguzi inakuathiri nini?

Anonymous said...

Kupanga ni kuchagua na kuyatenda yaliyochaguliwa yanachukua muda siyo kukurupuka tu. Hivyo CCM na viongozi wake wanaendelea kutekeleza mambo yaliyomo kwenye ilani ya chama na ambayo mengi wameshayamaliza na mengine ndiyo wanayafanya muda huu.