Alitangaza kuachana na siasa za chama tawala jana nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, akidai hatua yake inatokana na CCM kutofuata na kuheshimu Katiba. “Kuanzia leo,(jana) naachana na CCM kwa sababu siwezi kuhimili chama kinachoendeshwa bila kuheshimu Katiba, Katiba ndio inatuunganisha sisi wote, tunakuwa CCM kwa sababu tuna Katiba inayotuunganisha.
Nasema kuanzia sasa mimi najitoa kwenye CCM “Najua uamuzi wangu utawasumbua watu wengi, marafiki zangu, ndugu zangu, wazee wenzangu ambao wengine tunawasiliana mara kwa mara na hata vijana wengi.
Lakini ni uamuzi ambao ni lazima niufanye kwa sababu vinginevyo mimi nitajisaliti mwenyewe,” alisema. Kingunge ambaye amekuwa ndani ya chama tawala kwa takribani miaka 61, alisema hadharani kuwa hakusudii kujiunga na chama kingine cha siasa, zaidi ya kuhubiri kuwa, yeye kwa sasa ni muumini wa mabadiliko.
“Nimeanzia TANU, nimekuwa mwanaharakati wa kutafuta Uhuru mpaka tumeupata na mwanaharakati wa kuijenga Tanzania mpya. Naamini ukiingia katika chama lazima ufuate nidhamu ya chama, na nidhamu ni kufuata katiba.
Alipoulizwa kama Edward Lowassa angeteuliwa na CCM kuwania urais bado angeweza kuhama chama hicho, Kingunge alishindwa kufafanua vyema, zaidi ya kusema aliamua kumuunga mkono Lowassa kwa sababu alimuona ana sifa ya kukubalika ndani na nje ya CCM.
HABARI LEO
3 comments:
Mbona hyo mzee ni miongoni mwa watu waionunuliwa na lowasa siku nyingi tu. Yeye anasema kaondoka CCM kwa kuwa imeshindwa kufuata katiba, sasa huyo mgombea anaemuunga mkono yaani lowasa huo uteuzi wake wa kuwa mgombea pekee wa uraisi kupitia ukawa na chadema umepatikana kwa uvunjifu mkubwa wa katiba hadi kupelekea aliekuwa katibu mkuu wake Dr slaa kukikacha chama kwa hasira. Sasa utaona huyu mzee ni mnafiki na anajaribu kupotosha umma nini hasa kilochomfanya kuondoka CCM. Mabadaliko gani anayoyaona kwa lowasa kama si ufisadi mtupu. Wale viongozi wa CCM walioendelea kumuunga mkono lowasa hadi sasa wapo taabani hofu imewajaa kutokana jinsi magufuli anavyokubalika na wananchi na jinsi anavyoelekea kushinda uchaguzi wakati lowasa anasua sua na kampeni zake kitu ambacho hasa kilicho mpelekea kikunge atangaze kuuchana na CCM wakati huu ili kujaribu kumuokoa tajiri wake lakini ameshachelewa kwani tayari watanzania wanafahamu kuwa kikunge ni miongoni wa mwa wa watu walionunuliwa na lowasa katika mbio zake za kulazimisha kuwa raisi.
Alikuwa mtetezi mkubwa wa SOCIALISM ambayo ilitufanya tuwe masikini. Jee? Hiyo miaka 61 ambayo yeye alinufaika alikuwa anafuata katiba gani? amesaliti Socialism!
Ni mkumbo ule ule wa wanaona hawana nafasi tena katika CCM mpya ndiyo maana wanatimua mbio. Hakuna ajenda ya maana na sababu wanazotoa hazina msingi wowote.
Post a Comment