ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 11, 2015

TANZANIA YAFUNGWA GOLI 1 NA MALAWI LAKINI YAPITA SASA KUKUTANA NA ALGERIA

Mbwana Samata (kushoto) na Thomas Ulimwengu wakishangilia goli la pili lililofungwa na Ulimwengu
Mbwana Samata (kushoto) na Thomas Ulimwengu wakishangilia goli la pili lililofungwa na Ulimwengu wakati Stars ikicheza dhidi ya Malawi kwenye uwanja wa Taifa

Timu ya Tanzania Taifa Stars leo imefuzu kusonga mbele baada ya kufungwa goli 1-0 na Malawi goli lililopatikana katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 43 ya mchezo goli lililofungwa kifundi nje ya 18 na mchezaji machachali wa Malawi John Banda anayevaa jezi nambari 7.

Katika mchezo huo uliochezewa katika uwanja wa Kamuzu jijini Blantyre nchini Malawi, Tanzania ilicheza mchezo wa kujihami huku wakifanya mashambulizi ya kuvizia wakiwa wamemuacha mbele mchezaji Mbwana Samata karibu muda wote wa mchezo.

Katika kipindi cha kwa golikipa wa Taifa stars ameokoa magoli mengi ya wazi kama si umahili wake Tanzania tungekua tunazungumuza vingine sasa.

Ukiangalia kiuchezaji Tanzania haikucheza vizuri kwenye mechi labda waliingia dimbani wakijua kazi yao ni moja tu ya kulinda magoli yao 2 waliyoyapata kwenye mechi yao ya kwanza iliyochezwa siku ya Juamtano kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar siku ya Jumatano na kuibamiza Malawi kwa goli 2-0.

Kitu kingine katika mchezo huo waamuzi walikua wakionekana dhahili wakiipendelea Malawi, kwa mfano kuna mpira wa kurushwa aliutoa mchezaji wa Malawi lakini kwa mshangao wa wengi wakapewa Malawi kurusha, Kingine Malawi walitoa mpira wa kona baada ya mchezaji Thomas Ulimwengu kumgongesha mpira beki wa Malawi na kutoka kona mbele ya mshika kibendera lakini mshika kibendera huyo akaamuru iwe goal Kick. Jambo lingine ni la refa kutoa kadi za njano kwa wachezaji wawili wa Tanzania kwa nyakati tofauti kipindi cha kwanza huku akishindwa kutoa kadi za njano kwa wachezaji wa Malawi kwa makosa kama yale yaliyowapatia wachezaji wa Tanzania kadi za njano.

Kitu kingine ambacho Vijimambo ilikiona katika mchezo huu ni pale wachezaji wawili wa Tanzania Thomas Ulimwengu na Mbwan Samata walipopata kadi za njano kwa kujitakia wenyewe. wachezaji hawa walichezewa rafu kwa nayakati tofauti kipindi cha pili karibia na mpira kumalizika lakini cha ajabu ni kwamba walipoletewa machela ya kuwatoa uwanjani baada ya kuwa chini kwa muda mrefu walikataa kupanda na kunyanyuka kutaka kuendelea na mchezo kitu kilichopelekea refa kuwazawadia kadi za njano. 

Kosa kama hili ni kwa wachezaji kama hawa wanaolilia kila siku kucheza ulaya ni la kijinga sana, kama wangelipanda machela na kutolewa nje wasingepata kadi na bado wangerudi uwanjani na kuendelea na mpira bila madhara yeyote. Wachezaji hawa inabidi wajifunze mechi zijazo kwamba kadi zoa za njano zinaweza siku nyingine zikaigharimu timu.

Mpira wa wa Timu ya Taifa ulibadilika mwisho kwenye dadkika ya 76 alipoingia Mrisho Ngassa na kuiongezea uhai safu ya ushambuliaji na kufanya mpira kuchezewa upande wa Malawi kwenye dakika 10 za mwisho.

Vijimambo inatoa pongezi kwa Taifa Stars kwa hatua iliyofikia na tunakupongeza kocha Charles Mkwasa na jopo lako kwa kuionyesha mwanga wa soka la Tanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Tuombe Mungu . Algeria ni hadithi nyingine. .