Friday, October 23, 2015

UBUNGO WAMPOKEA DK. MAGUFULI KWA FURAHA TELE

 Wakazi wa Ubungo wakimshangilia kwa shangwe mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli.
 Wananchi wakiwamtandikia apite.

4 comments:

Anonymous said...

Nani kama maghufuli? Hakuna mpaka hivi sasa. Magufuli anakubalika , sera zake zinakubalika, watu wanamuamini anachokisema, hanaskendal au doa katika utumishi wake iliimradi kama kutakuwa hakuna mchezo mchafu siku ya uchaguzi hapana shaka Magufuli ndie raisi mpya wa Tanzania. Kinachokera kwa upande wa upizani kila kukicha kulalamika na kuwatia hofu wafuasi wao na watanzania kwamba wataibiwa kura jamani? Ukiangalia wao wapinzani ndio waliokuwa hawapo serious wa kuzitafuta kura . jinsi walivyokuwa wakifanya kampeni zao kama vile walikuwa wakitegemea kuna kajishotikati fulani hivi wanataka kuja kukitumia ili kushinda uchaguzi. Tofauti na magufuli alionekana kabisa yupo very serious katika kampeni zake kwa kuhakikisha anafikisha ujumbe wake wa kuomba kura kwa kumfikia mlengwa kwa macho na kuwapa fursa wapiga kura hao kumuelezea matatizo na matarajio yao . Magufuli amezunguka karibu kila kona ya Tanzania akiomba kura bila ya kujali nani anamuomba kura ilimradi alikuwa akiomba kuwatumikia watanzania tena unyenyekevu bila ya kujali itikadi zao za chama na tunaimani ikitokezea magufuli kuchaguliwa kuwa raisi haitakuwa surprise wala kutia shaka ushindi wake . wapinzani waache kuwaaminisha wafuasi wao kuwa wataibiwa kura kwani timu iliojiandaa vyema ndio yenye nafasi kubwa ya ushindi . Wapinzani iwaweke tayari wafuasi wake kuyakubali na kuyapokea matokeo ya kura kwa amani na kuendelea kulijenga taifa . Mungu ibariki Tanzania yetu. Amen.

Anonymous said...

Mimi namkubali Lowassa kuwa ni mkweli na sio mtu wa kupayuka.kwasababu siasa ni kuleta maendeleo kwa wananchi sio matusi wala kejeli. Pia nitampigia kura kutokana ataileta katiba ya Warioba ambayo sisi wananchi ndio itatutoa shimoni. Hebu angalia leo mtu unafanya kazi bila mkataba na tajiri anakutuma mambo yasiokuwa ya kikazi lakini utafanya kutokana hutaki kuikosa kazi yako. ndio sawa na wananchi hatuna katiba ndio maana ccm wanafanya watakavyo, na kuiba watakavyo sisi mlo mmoja kazi kuupata yaani mtu unakaa unajiuliza leo nitakula nini tumbo utasema lina chura huku viongozi wanakula milo mitano mpaka vyengine wanavimwaga.nikitakacho mimi ni katiba itakayoleta heshima kwa wananchi na viongizi wakikosea ili tuweze kuwajibisha na kuwa mwisho wa ufisadi.

Anonymous said...

Magufuli ni rais mteule na kesho atathibishwa.

Anonymous said...

Lowassa ndo Rais