ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI DAR SHWAAAAAAARI

 Hali imekuwa shwari katika Jiji la Dar es Salaam hasa wakati wa upigaji kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais wa Awamu ya Tano. Jiji hilo lenye pilikapilika nyingi za maisha mfukuto mkubwa wa kisiasa lakini hali haikuwa hivyo bali ilitawaliwa na amani kila mahala. Pichani ni baadhi ya barabara zikiwa hazina misururu ya magari na vyombo vingine vya moto kama ilivyozoeleka.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Hali ilivyokuwamchana wa leo  katika barabara za Morocco na Morogoro eneo la Magomeni Dar es Salaam.
 Kwenda Kinondoni kutoka Magomeni Mataa

 Kwenda Ilala, eneo la Mataa Magomeni
 Eneo la Banana Jimbo la Ukonga Dar
Hata wafanyabiashara hawakuwepo Banana, Ukonga Dar

3 comments:

Anonymous said...

nasikia raha kweli kweli.nakubaliana na wewe leo hii jumapili tarehe 25 octoba 2015 siku ya uchaguzi mkuu wa tanzania,mkoa mzima wa dar-es-salaam ulikua kimya sana,tena kupita kiasi.kwa ujumla asilimia 95 ya maduka yote yalifungwa,machinga woote safari vituoni ili kushiriki kumchagua mheshimiwa diwani,mheshimiwa mbunge na mheshimiwa rais.soma uyasikie niliyoyaona.mimi nilijihimu kituoni kwangu mnamo saa kumi alfajiri.pale niliwakuta waliotangulia! na nikapewa namba 55 kwa msingi itakapoanza foleni saa 1 asubuhi,tuliowahi tuchukue nafasi zetu.makarani wa tume walianza kuingia saa 1.05 na shughuli ikaanza rasmi saa 1.36 hivi.kwa ujumla maafisa hawa walikua wakimya sana na watulivu.sasa nilichohuhudia: NI KUHAMASIKA WA KUNDI KUU LA VIJANA KATIKA KUPIGA KURA,HAIJAWAHI KUTOKEA. YAANI NIMEWAONA.NI WENGI,NI WENGI,NI WENGI UCHAGUZI HUU VIJANA NDIYE WATAKAYETOA MSHINDI WA UCHAGUZI WA URAIS ,NAAPA. UPANDE WA WAZEE,INASIKITISHA,NIMEWASHUHUDIA SI ZAIDI YA 15 KWA KUPEPESA MACHO.WAMECHOKA,WAMEKATA TAMAA,WANAMLILIA KINGUNGE NGOMBARE-MWILU NITAONGEA MENGI BAADA YA MHESHIMIWA KUAPISHWA.NAITWA KIUNGWA MILEMETWA.

Anonymous said...

kweli shwaaali,jana tumepiga kura zetu kwa amani na utulivu.ilikua inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.idadi ya wapiga kura ilikua ni kubwa mno,kubwa sana,na kwa hiyo foleni zilikua ndefu mno.ilibidi wale ambao afya zao haziruhusu kusimama kwa muda mrefu wakamate namba kwa aliye mbele yake.kwa ujumla wapiga kura tulionyeshana upendo wa hali ya juu,kuchat,kucheka,kuwaelekeza wale waliochelewa.ulinzi wa polisi -doria ulikua mchache na kwa jumla hatukuuhitaji.wananchi wamepiga kura na kisha wameendelea na maisha mengine.Ila niongee kitu kimoja kilichonipendeza sana sana,nacho ni uwepo wa vijana katika zoezi hili.robo tatu ya wapiga kura niliowashuhudia nilipopigia kura[shuleni,palikua na milango nane] walikua ni vijana.kisha kwa mapenzi yangu,nikitumia usafiri wa mwanangu[namshukuru] nilitembelea maeneo mengi tuu nikiendelea kushuhudia foleni ndefu sana.NI WAZI MABADIRIKO YAMEKUJA TANZANIA.VIJANA WAMEAMKA,WAMEKUA WA MFANO.MHESHIMIWA ATAKAYEPITA URAIS,AWE LOWASSA,AWE MAGUFULI AJUE WAZI KABISA KWAMBA KUPITA KWAKE NI KUTOKANA NA MWAMKO MKUBWA WA VIJANA WATANZANIA,MSIJE MKAWAANGUSHA WANA MATUMAINI MAKUBWA SANA NA TANZANIA MPYA.

Anonymous said...

Jidanganyeni na kejeli zenu wakati wenzenu karibu wanatangaz ufalme wao tena. #Hapa ni kazi tu.