Na Mwandishi
wetu, Dar es salaam
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai yaliyotolewa na
Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya kuwa wanaudai Mfuko jumla ya
shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni, 2015.
Akizungumza
jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospital hiyo ya Rufaa
Mkoa wa Mbeya hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo unalipa madai
baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.
Amesema
madai ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015.
Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko tarehe 4/11/2015
ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari hadi Agosti
2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai mengi
ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu mkubwa hali
inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo kuwapigia simu
wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha Mhando
amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao wamekuwa bado
wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa haitawaonea haya kuwafutia
usajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Amesema
Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa na
Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa wanachama na
Watanzania kwa ujumla.
Wakati
huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa huduma
wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma nzuri ama za
kuridhisha kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla kwa kisingizio cha
kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa vifaa tiba na vitendanishi
pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya vituo.
Watoa huduma
hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma katika maeneo yao
kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai ambayo wametibia
wanachama wake.
Amesema
taarifa hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi wa
vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta chuki baina
ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina dhamana ya kuwatibia.
Hata hivyo
Mhando amekanusha kuwa wao ndio kikwazo ama sababisho la huduma mbovu
katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada mbalimbali
ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na Serikali katika
kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja wapate huduma
zinazostahili.
MWISHO.
(Imeandaliwa
na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment