Handeni. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Handeni Mjini wamempigia kura na kumchagua tena mgombea ambae alishinda awali Omari Abdallah Kigoda katika uchaguzi uliofanyika wilayani humo leo baada ya kamati kuu ya CCM Taifa kutaka urudiwe.
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Dk Maua Daftari alisema kuwa wajumbe wote kwenye mkutano walikuwa 690 na waliopiga kura ni 660 na uchaguzi ulikuwa wa wazi na haki na hakukuwa na tatizo lolote.
Alisema Omari Kigoda amepata kura 402 na mgombea mwenzake Hamisi Mnondwa alipata kura 257 huku kura moja ikiharibika na kufanya jumla ya kura zote kuwa ni 660 hivyo kumtangaza Omari kuwa mshindi katika kura halali 259.
Awali kabla ya uchaguzi huo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Taifa Abdallah Bulembo alisema kuwa sababu kubwa ya kurudiwa uchaguzi huo ni kutokana na mshindi wa kwanza na aliyemfuatia kushindwa kuvuka nusu ya idadi ya wapiga kura hivyo hawakufika katika vigezo vinavyotakiwa.
Mgombea huyo anatarajiwa kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Handeni Mjini kesho na kuirudisha ambapo tarehe tano wataanza kampeni rasmi.
3 comments:
Hii imekuwa ndio tija kwa Tanzania kulipeleka taifa pasipokues! nini kinamfanaya akubalike kugombea ubunge wakati wote alikuwa wapi kwani angeliingia kwenye kinyanganyiro na baba yake akiwa hai isingewezekana!1 huku kupeana nafasi za uongozi hakutaisaidia Tanzania kuvuka kwenye wimgi la umasikini, hakuna watu wengine katika chama wanaoweza ila huyu, hapo zzimetumika zile zile za kubandika kura na sidhani kama imefanyika itakiwavyo, sina hiana ila kwa ujumla ukitizama mtiririko ni dili ya umimi, haya twende!!
We mtoa mada wa 11:14am...acha kelele kama ngedere subiri uchaguzi upigwe wananchi wa handeni waamue . Kwani kupitishwa na chama chake cha CCM ndio kishachaguliwa kuwa mbunge? Si imeshatokezea mara kadhaa kwa CCM kumsimamisha mtoto wa marehemu mbunge kama mgombea wao na kushindwa uchaguzi katika ngazi ya Taifa. Licha ya CCM kumsimamisha huyo mtoto wa marehemu mbunge maamuzi ya mwisho wanayo wananchi wenyewe wa handeni na kuwa mtoto wa kiongozi sio dhambi inayomzuia mtu kufuata nyayo za mzee wake kuwakilisha wananchi kama huyo mtu anauwezo wakufanya hivyo.
Tz kuna uchaguzi au kiini macho
Post a Comment